IQNA

Mazishi ya Kiongozi Shahidi yameibadili taswira ya Iran duniani

17:10 - July 10, 2026
Habari ID: 3482466
IQNA – Mazishi makubwa na yenye adhama ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, yaliyovuta mamilioni ya waombolezaji, hayakuwa tu hafla ya kitaifa, bali pia yamekuwa nukta ya mageuzi katika kuijenga upya taswira ya Iran katika medani ya kimataifa.

Hayo yamesemwa na Yahya Jahangiri, mtafiti na mwanaharakati wa kimataifa, katika mahojiano yake na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)

Amesema kwamba kile kilichojengeka leo katika maoni ya umma duniani kuhusu Iran ni, zaidi ya yote, matokeo ya uwepo wa wananchi wenyewe na simulizi lililopelekwa ulimwenguni kuhusu muqawama, mshikamano, na uthabiti wa taifa la Iran.

Akirejea vipengele vya kimedia na kijamii vya misafara mikubwa ya mazishi ya Kiongozi Shahidi, Jahangiri ameutaja msiba huo kuwa ni miongoni mwa matukio muhimu zaidi ya miaka ya hivi karibuni katika kuunda taswira ya taifa. Amesema kuwa katika dunia ya leo, mataifa hutambulika kwanza kwa picha inayoundwa kuyahusu na vyombo vya habari, simulizi, na matukio ya kihistoria, kabla hata ya kutambulika kwa uhalisia wa hali ya ardhini.

Ameongeza kuwa watu wengi duniani hawajawahi kuiona nchi fulani kwa macho yao wenyewe, na kwa hivyo mtazamo wao juu ya nchi hiyo hujengwa na taswira hiyo ya kiakili.

“Hata wale waliowahi kuishi au kutembelea jamii fulani, wakati mwingine hubadilisha mitazamo na dhana zao wanapokutana na matukio makubwa ya kihistoria,” Jahangiri aliongeza.

Amesema kuwa baadhi ya matukio ya kihistoria yana uwezo wa kubadili kabisa mizani ya fikra za maoni ya umma.

“Wakati mwingine ushindi, wakati mwingine kushindwa, na wakati mwingine tukio la kihistoria hutengeneza sura mpya kabisa ya taifa katika fikra za ulimwengu. Kwa mtazamo huu, mazishi makubwa ya Kiongozi Shahidi yanapaswa kuhesabiwa kuwa ni miongoni mwa matukio muhimu zaidi ya miaka ya hivi karibuni katika kujenga taswira; tukio ambalo limeijengea Iran sura tofauti na ya kipekee katika medani ya kimataifa.”

Amebainisha kuwa ushiriki mkubwa wa wananchi, hisia za pamoja, adhama ya hafla yenyewe, na mwangwi wake mpana, vyote kwa pamoja viligeuka kuwa simulizi la kimataifa.

Jahangiri alieleza kuwa, mbali na uwepo wa wananchi, nafasi ya wanaharakati wa vyombo vya habari, wanaharakati wa kitamaduni na kisanii, watayarishaji wa maudhui, na wote waliobeba taswira hiyo na kuifikisha ulimwenguni pia ilikuwa ya msingi sana. Kwa mujibu wake, wao walichukua nafasi muhimu katika kuuweka msimamo huu ndani ya kumbukumbu ya maoni ya umma duniani.

Akirejea uzoefu wake akiwa nje ya nchi, Jahangiri alisema:

“Nimekuwa nje ya Iran tangu Januari, na niliona kutoka nje jinsi mazingira ya siku zile nchini Iran yalivyokuwa yamejaa maswali na sintofahamu. Lakini kuzuka kwa Vita vya Tatu vya Kulazimishwa kulibadili kimsingi hali ya maoni ya umma.”

Baada ya kuuawa shahidi Kiongozi huyo na juhudi kubwa zilizofanywa katika kusimulia vita hivyo, amesema:

“Ninaamini kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilipata mkono wa juu katika medani ya ‘vita vya simulizi’.”

Akiashiria kuwa bado haujapita muda mrefu tangu kufanyika kwa mazishi hayo makubwa ya Kiongozi Shahidi, mtafiti huyo alisisitiza kuwa:

“Sizungumzi tu kama mchambuzi, bali pia kama shahidi wa moja kwa moja wa hali halisi, ninaweza kusema kuna dalili wazi za mabadiliko makubwa katika maoni ya umma duniani kuhusu Iran.”

Akieleza aliyoyaona mwenyewe kuhusu mabadiliko ya mitazamo ya watu wa nchi mbalimbali kuelekea Iran, Jahangiri alisema:

“Leo, kila ninapoingia sokoni, dukani, au katika mkusanyiko wa watu wa kawaida, mara tu wanapogundua kuwa mimi ni Muirani, angalau hunipokea kwa ishara ya ‘like’ na maneno ya heshima. Tabia hii inaweza kuonekana kuwa rahisi juu juu, lakini kwa mtazamo wa kijamii ina maana kubwa sana, na inaonesha kuwa Iran imekuwa ‘nembo’ katika fikra za watu wengi.”

3498182

captcha