IQNA

Al-Khazali: Kiongozi Shahidi Alikuwa Mshika Bendera wa Haki Katika Zama Zetu

20:50 - July 08, 2026
Habari ID: 3482460
IQNA – Katibu mkuu wa Harakati ya Asaib Ahl al-Haq nchini Iraq, Sheikh Qais Al-Khazali, amesema kuwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, alikuwa “mshika bendera wa haki katika zama zetu.”

Akihudhuria hafla rasmi ya kupokea mwili wa Kiongozi huyo Shahidi katika Uwanja wa Ndege wa Najaf Jumanne usiku, Al-Khazali alisema: “Tunatoa rambirambi zetu kwa Waislamu wote na watu huru duniani kote kutokana na msiba huu mzito. Tunamuomba Allah atujaalie tuwe miongoni mwa wale watakaolipiza damu ya Sayyid Al-Khamenei, damu ya babu yake Imam Hussein, na damu ya kila aliyedhulumiwa, pamoja na Imam mshindi kutoka Ahlu Bayt ya Muhammad (amani na rehma ziwe juu yao).”

Akaongeza: “Leo tunapokea mwili huu mtakatifu katika mji mtukufu wa Najaf, ardhi ya babu yake Imam Ali (amani iwe juu yake), na kesho Iraq yote itamuaga; Waislamu wake, Wakristo na Wamandaea; Waarabu wake na Waturukmani wake; Masunni wake na Mashia wake.”

Msafara wa mazishi wa Kiongozi Shahidi, Ayatullah Khamenei, unaendelea katika mji mtukufu wa Najaf. Msafara huo utaendelea pia katika mji mtukufu wa Karbala mchana wa Jumatano.

Al-Khazali alisema kuwa “Iraq nzima itashiriki katika mazishi ya mwanadamu huyu, ambaye alikuwa mshika bendera wa haki katika kutenganisha haki na batili,” na kuongeza: “Allah ataithibitisha haki kwa maneno Yake na ataizima batili, hata kama wahalifu wataichukia vipi, na sisi tutalipiza kisasi dhidi ya wahalifu.”

3498157

Habari zinazohusiana
captcha