IQNA

Kiongozi Shahidi ni nembo ya heshima, utukufu, na mapambano

16:22 - July 11, 2026
Habari ID: 3482469
Shahidi
IQNA – Kamati za Muqawama wa Palestina (Palestinian Resistance Committees) zimesisitiza kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Khamenei, atabaki kuwa alama ya heshima, utukufu, mapinduzi, na muqawama.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, Kamati za Muqawama (mapambano) wa Palestina zilieleza kuwa urithi wa Kiongozi Shahidi utaendelea kuwepo katika dhamiri ya waumini na watu huru, kwa mujibu wa taarifa kutoka Kituo cha Habari cha Palestina.

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa kuuawa shahidi Ayatullah Seyed Ali Khamenei hakutafanikiwa kuizima harakati ya Mapinduzi ya Kiislamu.

“Damu ya shahidi Ayatullah Khamenei imewasha moto wa mapinduzi na kuifanya iwe yenye azma zaidi na imara zaidi katika kukabiliana na nguvu za ubeberu wa kimataifa, Uzayuni, Marekani, na Magharibi kwa jumla,” ilieleza taarifa hiyo.

Iliyongeza kuwa Shahidi Khamenei aliishi kama mujahid na kiongozi mwenye haki na busara, na alikufa shahidi akiwa amesimama imara katika misingi yake, bila  kusalimu amri wala kulegeza msimamo au kuingia katika makubaliano ya kuondoka katika mkondo wa haki.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Kiongozi aliyeuawa shahidi aligeuza suala la Palestina kuwa itikadi ambayo haiwezi kupuuzwa.

Ikibainisha kuwa hafla za mazishi na kumuaga Shahidi Ayatullah Khamenei zimekuwa ni kielelezo cha kihistoria cha uaminifu na alama ya utukufu, taarifa hiyo iliongeza kuwa kuawa shahidiviongozi hakizuii njia ya mapambano, bali badala yake huipa njia hiyo azma yenye nguvu zaidi, uthabiti wa mizizi mirefu, na imani ya ndani zaidi.

4363234

Habari zinazohusiana
captcha