mazishi ya imam khamenei

IQNA

IQNA – Katika Khitma ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, iliyofanyika katika Haramu Tukufu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, Qari mashuhuri wa Iran, Ustadh Ahmad Abolqassemi, aliongoza usomaji wa aya za 64 hadi 71 za Surah An-Nisa pamoja na Surah Al-Fatiha.
Habari ID: 3482511   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, amesema kuwa misafara ya mazishi ya Kiongozi Shahidi, iliyohudhuriwa na mamilioni ya watu, imedhihirisha kikamilifu upana wa huruma, udugu, na mshikamano uliopo kati ya mataifa mawili ya Iraq na Iran.
Habari ID: 3482505   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19

IQNA – Msomaji mahiri wa Qur’ani na jaji wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani kutoka Yemen amesema kuwa yeyote anayetafakari mafunzo ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, atatambua kuwa aliishi maisha yake yote ndani ya ulinzi na mwongozo wa Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3482504   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/18

IQNA – Washindi wa duru ya kwanza ya Tuzo ya Kimataifa ya Ushairi ya “Imamu Shahidi” walitangazwa na kutunukiwa katika hafla iliyofanyika mjini Tehran siku ya Jumanne.
Habari ID: 3482491   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/15

IQNA – Uwepo wa mamilioni ya waumini katika misafara ya mazishi iliyofanyika nchini Iran na Iraq kwa ajili ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, unabeba ujumbe muhimu, wa kina na wenye nguvu.
Habari ID: 3482483   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14

IQNA – Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) limeandaa tuzo ya 12 ya Kimataifa ya Arbaeen mwaka huu.
Habari ID: 3482480   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/13

IQNA – Askofu wa Kanisa la Othodoksi la Bishkek, nchini Kyrgyzstan, amemwelezea Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, kama kielelezo hai cha maadili na misingi ya Kiungu.
Habari ID: 3482475   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/12

IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, ameeleza shukrani zake za dhati kwa mahudhurio “ya kustaajabisha, yenye kuvunja nguvu za adui na ya kihistoria” katika mazishi ya Kiongozi Shahidi, akisisitiza kuwa malipo ya kisasi dhidi ya “watenda jinai wauaji waliodhalilika” ni jambo la yakini.
Habari ID: 3482472   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/11

IQNA – Msafara mkubwa wa kinembo wa maombolezo wenye anwani ya “Kumuaga Imam Khamenei” umefanyika huko Kargil, India, siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3482470   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/11

IQNA – Kamati za Muqawama wa Palestina (Palestinian Resistance Committees) zimesisitiza kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Khamenei, atabaki kuwa alama ya heshima, utukufu, mapinduzi, na muqawama.
Habari ID: 3482469   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/11

IQNA-Hafla ya mapokezi na mazishi ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahid wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Husayni Khamenei, pamoja na mashahidi wa familia yake, ilifanyika siku ya Alhamisi, tarehe 9 Julai kuanzia Mtaa wa Imam Ridha (AS) kuelekea Haram Tukufu ya Ridha (AS) mjini humo.
Habari ID: 3482468   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/10

Shughuli ya kuusindikiza mwili mtukufu wa Imamu Mujahid Shahidi, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (qaddasallahu nafsahu al-zakiyyah) ilifanyika siku ya Jumatano, tarehe 8 Julai , katika mji mtukufu wa Najaf al-Ashraf, kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi waombolezaji wa Iraq. Baada ya msafara wa mazishi, Ayatullah Sayyid Muhammad-Taqi al-Hakim, mmoja wa wanazuoni wa Iraq, aliswalisha Swala ya Maiti ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ndani ya haram tukufu ya Amir al-Mu’minin Ali (AS).
Habari ID: 3482467   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/10

IQNA – Mazishi makubwa na yenye adhama ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, yaliyovuta mamilioni ya waombolezaji, hayakuwa tu hafla ya kitaifa, bali pia yamekuwa nukta ya mageuzi katika kuijenga upya taswira ya Iran katika medani ya kimataifa.
Habari ID: 3482466   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/10

IQNA – Msomi mwandamizi wa Bahrain amesema kuwa umoja katika mtazamo wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, si nembo tu ya kisiasa; bali ni neno-msingi katika mkakati wake wa kistaarabu wa kurejesha izza, heshima na mamlaka kwa Ummah wa Kiislamu.
Habari ID: 3482465   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/10

IQNA – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa shukrani za dhati kwa wananchi na viongozi wa Iraq kwa ukarimu wao katika kuandaa msafara wa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, wakati mamilioni ya waombolezaji walipofurika katika mitaa ya Najaf na Karbala katika dhihirisho la kihistoria la mshikamano.
Habari ID: 3482464   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/10

IQNA – Baada ya siku kadhaa za misafara ya mazishi na hafla za kuaga nchini Iran na Iraq, Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amezikwa kandokando ya haram tukufu ya Imam Ridha (AS) mjini Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3482463   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/10

IQNA-Katika ujumbe uliotolewa mapema leo Alkhamisi, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Brigedia Jenerali Esmail Qaani ametoa shukrani kwa taifa na serikali ya Iraq kwa maandalizi mazuri ya mazishi ya Kiongozi aliyeuawa shahidi wa Mapinduzui ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei na watu wa familia yake.
Habari ID: 3482462   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/09

IQNA – Katibu mkuu wa Harakati ya Asaib Ahl al-Haq nchini Iraq, Sheikh Qais Al-Khazali, amesema kuwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, alikuwa “mshika bendera wa haki katika zama zetu.”
Habari ID: 3482460   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/08

IQNA – Swala za Maiti kwa ajili ya miili ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na wanafamilia yake imeswaliwa katika harimu tukufu ya Imam Ali (AS) mjini Najaf, Iraq, siku ya Jumatano asubuhi.
Habari ID: 3482457   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/08

IQNA – Uwanja wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini (RA) mjini Tehran umekuwa uwanja wa kukutania nyoyo zilizokusanyika kati ya tarehe 4 na 5 Julai, 2026, kwa ajili ya kumuaga kwa heshima za mwisho Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Habari ID: 3482456   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/07