iqna

IQNA

sala ya ijumaa tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaandaa ramani ya njia ya ushirkiano na nchi zingine kwa kuzingatia maslahi yake ya taifa.
Habari ID: 3474832    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/21

TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, adui anaihitajia zaidi Iran katika mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna Austria na kusisitiza kuwa, inabidi tusimame imara na kwa ghera katika vita vya kidiplomasia.
Habari ID: 3474806    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/14

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa: Kambi iliyoasisiwa na shujaa Shahidi Qasem Soleimani katika vita vikali dhidi ya batili itawaangamiza kabisa Wamarekani na mamluki wao katika eneo hili la Magharibi mwa Asia.
Habari ID: 3474777    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/07

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa msingi wa mazungumzo ya nyuklia JCPOA yanayofanyika mjini Vienna ni kuondolewa kwa mpigo vikwazo ilivyowekewa Iran.
Habari ID: 3474687    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/17

Hatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa Iran ya leo ndiyo nchi yenye nguvu zaidi katika eneo la Magharibi mwa Asia, na iko katika nafasi ambayo hakuna nchi inayothubutu kuishambulia.
Habari ID: 3474659    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/10

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa, taifa la Iran halitokubaliana na chochote katika mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna Austria ghairi ya kuondolewa vikwazo vyote vya kidhalimu lilivyowekewa taifa hili la Kiislamu na madola ya kibeberu.
Habari ID: 3474632    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/03

TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezinasihi nchi za Ulaya kutotoa mhanga maslahi yao ya kitaifa kwa manufaa na malengo haramu ya watawala wa Marekani na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3474601    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/26

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema leo masuala ya Iraq na Afghanistan ni muhimu kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3474545    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/12

TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa Iran iko tayari kuingia kwenye mazungumzo ambayo matokeo yake ni kuondolewa vikwazo vyote na kwamba haikubali mazungumzo yasiyo na mwelekeo.
Habari ID: 3474516    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/05

TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, harakati zinazofanywa na mabeberu kwa sasa zinalenga kuvuruga amani na usalama.
Habari ID: 3474488    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/29

TEHRAN (IQNA)- Baada ya kusitishwa kwa muda wa takribani miezi ishirini jijini Tehran na katika miji na maeneo mengine ya Iran kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, Swala ya Ijumaa imefanyika leo mjini Tehran ikishirikisha matabaka mbalimbali ya wananchi.
Habari ID: 3474458    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/23

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, amesema, kaulimbiu ya "Mauti kwa Marekani" imetimia kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Majlisi ya 11 ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na uchaguzi mdogo wa Baraza la 5 la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Habari ID: 3472492    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/21

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, lau kama si Mapinduzi ya Kiislamu hii leo Marekani na utawala haramu wa Israel zingekuwa zinaidhibiti Iran na ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3472447    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/07

Khatibu wa Sala ya Ijuma Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameilaani Marekani kwa kuanzisha njama mpya dhidi ya Waislamu kwa jina la "Muamala wa Karne" na kusema kuwa, njama hizo zitafeli na kushindwa tu.
Habari ID: 3472425    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/31

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi-Fard
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa mauaji yaliyofanywa na jeshi la kigaidi la Marekani dhidi ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni mwanzo wa kufukuzwa Marekani katika eneo hili la magharibi mwa Asia sambamba na washirika wake katika eneo kusambaratika.
Habari ID: 3472403    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/24

TEHRAN (IQNA) -Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa jana mjini Tehran, imeakisiwa sana na vyombo vya habari vya kigeni.
Habari ID: 3472382    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/18

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
THERAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pigo la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kwa adhama ya Marekani ni jambo ambalo limepelekea nchi hiyo ifedheheke na kuongeza kuwa: "Pigo hilo kubwa na lenye nguvu haliwezi kufidiwa kwa chochote na hivyo hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kuongeza vikwazo haiwezi kuondoa fedheha hiyo."
Habari ID: 3472379    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/17

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA) - Katibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amemtaja shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mratibu wa usalama na amani endelevu kupitia mapambano (muqawama).
Habari ID: 3472358    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/10

TEHRAN (IQNA) -Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran ameashiria matukio ya hivi karibuni katika nchi za Kiislamu na kusema kuwa, kuna ulazima kwa Waislamu kuwa macho mbele ya njama za maadui huku akitoa wito kwa Waislamu duniani kumtetea Sheikh Ibrahim Zakzaky wa Nigeria.
Habari ID: 3472290    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/20

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA) -Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kulikuwa na mpango hatari nyuma ya wazua ghasia za hivi karibuni nchini Iran ambapo ghasia hizo ziliratibiwa na uistikbari wa dunia miaka miwili iliyopita sambamba na kugawa silaha na kutoa mafunzo.
Habari ID: 3472240    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/29