iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Sala ya Ijumaa imeswaliwa jana katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) ambapo inakadiriwa kuwa Wapalestina 40,000 walishiriki katika sala hiyo.
Habari ID: 3473959    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/29

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kufanya chokochoko na mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya mji wa Quds (Jerusalem) na Msikiti Mtukufu wa al Aqsa mjini humo.
Habari ID: 3473942    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/24

TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu (IUMS) imetoa Fatwa inayobainisha kuwa, kuunga mkono Palestina ni jukumu la Kiislamu.
Habari ID: 3473922    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/18

Wapalestina karibu laki moja wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr Alkhamisi asubuhi katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao siku chache zilizopita wanajeshi wa utawala huo katili waliwashambulia kwa mabomu Waislamu waliokuwa wanasali ndani ya Msikiti huo.
Habari ID: 3473911    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/15

TEHRAN (IQNA)-Wapalestina karibu laki moja wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr leo Alkhamisi asubuhi katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao siku chache zilizopita wanajeshi wa utawala huo katili waliwashambulia kwa mabomu Waislamu waliokuwa wanasali ndani ya Msikiti huo.
Habari ID: 3473906    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/13

TEHRAN (IQNA)- Mabalozi wa kudumu wa nchini wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika Umoja wa Mataifa wametangaza azma yao ya kuhamisisha jamii ya kimataifa iunge mkono taifa la Palestina ambalo linakabiliwa na hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473899    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/11

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amemwandikia barua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumjulisha matukio na mabadiliko yanayojiri katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473894    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/10

TEHRAN (IQNA)- Ijumaa iliyopita tarehe 7 Mei askari wa utawala haramu wa Israel walivamia msikiti mtakatifu wa al-Asqa katika mji wa Quds (Jerusalem). na kuwapiga kikatili Wapalestina waliokuwa wanatekeleza ibada zao katika msikiti huo. Shirika la Hilali Nyekundu ya Palestina limesema Wapalestina wasiopungua 205 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.
Habari ID: 3473890    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/09

TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali hujuma ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa wakati Wapalestina walipokuwa katika eneo hilo takatifu.
Habari ID: 3473887    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/08

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani vikali hatua ya utawala haramu wa Israel ya kukata nyaya za vipaza sauti katika Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na kuzuia kuadhiniwa kwa kutumia vipaza sauti.
Habari ID: 3473816    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/15

TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) amesisitiza kuhusu udharura wa kuungana Waislamu katika kutangaza mwezi mwandamo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473795    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/09

TEHRAN (IQNA) – Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia Wapalestina ambao walikuwa wakiandamana katika Ukingo wa Magharibi kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.
Habari ID: 3473766    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/28

TEHRAN (IQNA)- Maeneo yote ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) yatakuwa wazi kwa waumini Waislamu kwa ajili ya ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473681    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/25

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza uchimbuaji chini ya Ukuta wa Nudba na Msikiti wa Al Aqsa ikiwa ni katika njama zake za kuuyahudisha mji wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3473621    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/04

TEHRAN (IQNA) - Sheikh Mohammad Hussein, Mufti Mkuu wa Quds (Jerusalem) ameulaani vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuzuia ukarabati wa Msikiti wa Al Aqsa.
Habari ID: 3473597    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/28

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Wananchi wa Yemen ameashiria kuendelea kuchimbwa mashimo na njia za chini kwa chini kuelekea katika msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu na kueleza kwamba, Waislamu wanapaswa kutumia nyenzo na suhula zote kukabiliana na njama hizo.
Habari ID: 3473483    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/23

TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya Wapalestina leo wamshiriki katika Swala ya Ijumaa katika kibla cha kwanza cha Waislamu, yaani Msikiti wa Al Aqsa ulioko mjini Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3473467    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/18

TEHRAN (IQNA)- Malefu ya Wapalestina wameshiriki katika Swala ya Ijumaa wiki hii katika Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel.
Habari ID: 3473360    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/14

TEHRAN (IQNA) – Utawala wa Kizayuni wa Israel umempiga marufuku naibu mkurugenzi wa Idara ya Wakfu ya Mji wa Quds (Jerusalem) kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa kwa muda wa miezi sita.
Habari ID: 3473330    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/05

TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Palestina amelaani kitendo cha kuruhusiwa ujumbe wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuingia ndani ya Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huku Wapalestina wakizuiwa kuswali katika msikiti huo.
Habari ID: 3473279    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/20