iqna

IQNA

IQNA- Swala ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika misikiti mbalimbali duniani, ikiwemo Msikiti wa Masjid al Al-Haram katika mji mtakatifu wa Makka, na Msikiti wa Al-Azhar nchini, iliandamana na dua kwa ajili ya Wa palestina wa Gaza na Msikiti wa Al-Aqsa.
Habari ID: 3480464    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/29

IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa wananchi wa Iran kuonyesha umoja na mshikamano wao wakati wa Siku ya Kimataifa ya Quds, akisisitiza kwamba kujitokeza kwa wingi wananchi katika siku hii kutaonyesha msaada usiotetereka wa Jamhuri ya Kiislamu kwa malengo ya ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3480446    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/27

IQNA – Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST) imetayarisha bango la Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu wa 1446 H sawa na 2025.
Habari ID: 3480437    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/25

IQNA – Siku ya Kimataifa ya Quds ni fursa ya kuonyesha msaada wa umma kwa  taifa la Palestina na ukombozi wa al-Quds, amesema afisa mwandamizi nchini Iran.
Habari ID: 3480435    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/25

IQNA – Jiji la Vienna, mji mkuu wa Austria, lilishuhudia maandamano makubwa yanayopinga kuendelea kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza. Waandamanaji walibeba mabango na vipeperushi vyenye maandiko, “Acha kuua watoto,” “Acha vita sasa,” na “Susia Israel."
Habari ID: 3480427    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/24

IQNA – Wakati ulimwengu wa Kiislamu ukikaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), Hissein Brahim Taha, amemuomba Mwenyezi Mungu aujali mwezi huu uwe "hatua muhimu” katika ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3480284    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/01

IQNA-Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vimemkamata na kumpiga marufuku Sheikh Najeh Bakirat, kiongozi mashuhuri wa Kiislamu Palestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa ulioko jijini Al Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3480246    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/21

Kadhia ya Palestina
IQNA-Mkuu wa Makao Makuu ya Intifada na Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran, Brigedia Jenerali Ramezan Sharif, amesisitiza umuhimu wa kupanga na kufanya juhudi za kufanikisha maandamano makubwa katika Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu.
Habari ID: 3480232    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/18

IQNA – Afisa mwandamizi wa Hamas alisema kuwa Operesheni ya kimbunga cha  Al-Aqsa ina matokeo makubwa ya kistratejia ambayo yatashuhudiwa hivi karibuni. 
Habari ID: 3480123    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/30

IQNA – Mkuu wa Ofisi ya Mashujaa, Waliojeruhiwa, na Mateka wa wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameelezea kuachiliwa kwa mateka wa Palestina kuwa sherehe ya kitaifa na alama ya umoja.
Habari ID: 3480105    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/27

Kadhia ya Palestina
IQNA-Baada ya kutangazwa makubaliano ya usitishaji vita huko Gaza, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii na kuandika: Subira na kusimama kidete kwa wananchi na Muqawama (mapambano ya Kiislamu) wa Wa palestina vimeulazimisha utawala wa Kizayuni kurudi nyuma.
Habari ID: 3480061    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/16

Muqawama
IQNA-Jeshi la Yemen limetangaza kwamba limeilenga kwa mafanikio Wizara ya Vita ya utawala haamu wa Israel na kuitwanga kwa kombora la balestiki.
Habari ID: 3480052    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/14

Diplomasia ya Muqawama
IQNA – Msimamo wa Yemen katika mhimili wa muqawama unatokana  na msingi wa Imani, Qur'an Tukufu na mwongozo wa Mwenyezi Mungu, amesema balozi wa nchi hiyo nchini Iran.
Habari ID: 3480032    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/11

Mtazamo
IQNA – Mchambuzi wa kisiasa wa Palestina amesema Shahidi Jenerali Qassem Soleimani aliona kadhia ya Palestina kama suala kuu la ulimwengu wa Kiislamu, ambalo linapaswa kuungwa mkono kwa njia yoyote ile.
Habari ID: 3480000    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/03

Jinai za Israel
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha A-Azhar cha Misri kimebainisha matumaini kwamba mwaka wa 2025 utakuwa mwaka wa ushindi na amani kwa Wa palestina wanaokabiliwa na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.
Habari ID: 3479990    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/01

Kadhia ya Palestina
IQNA-Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa wito wa kufanyika "hamasa kubwa ya umma" kwa lengo la kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3479949    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/24

Muqawama
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni unakodolea macho ya tamaa maeneo yote yanayopakana na ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu yakiwemo ya Syria na Misri na kusema kuwa, Netanyahu anatumia vibaya matukio ya Syria ili kutimiza njama hizo za muda mrefu za Kizayuni.
Habari ID: 3479899    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/14

Waungaji mkono Palestina
IQNA - Maelfu ya wananchi wa Yemen waliingia barabarani mjini Saada kutangaza uungaji mkono wao kwa mataifa ya Palestina na Lebanon na kulaani vitendo vya uchokozi vya utawala wa Israel dhidi ya Syria.
Habari ID: 3479896    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/14

Watetezi wa Palestina
IQNA-Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano mapya ya kila wiki katika mji mkuu Sana'a na miji kadhaa nchini humo kusisitiza uungaji mkono wao kwa Wa palestina wanaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel.
Habari ID: 3479868    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/07

Waungaji Mkono Palestina
IQNA - Mji mkuu wa Uingereza,  London siku ya Jumamosi ulikuwa eneo la mjumuiko mkubwa ulioandaliwa na waandamanaji wanaounga mkono Palestina.
Habari ID: 3479840    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/02