Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA) - Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge ameandika barua kwa Umoja wa Mabunge na Maspika wa Mabunge ya Nchi mbalimbali duniani na kuitaka jamii ya kimataifa kupaza sauti kwa pamoja ili kuondolewa haraka iwezekanavyo vikwazo vikiwemo vya kitiba vya Marekani dhidi ya wananchi wa Iran.
Habari ID: 3472550 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/10
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Mousavi amelaani shambulio hilo la kigaidi sambamba na kuwafariji wananchi na serikali ya Afghanistan pamoja na familia za waliouawa na kujeruhiwa katika hujuma hiyo.
Habari ID: 3472542 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/07
TEHRAN (IQNA) - Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ambayo yalikuwa yafanyike katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yameakhirishwa kutokana na kuenea kirusi cha Corona nchini Iran.
Habari ID: 3472536 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/06
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa maelekezo muhimu kuhusiana na mradhi yaliyoenea ya COVID-19 yanayosababishwa na kirusi cha corona humu nchini Iran.
Habari ID: 3472527 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/03
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya wanafunzi ya Waislamu yameakhirishwa.
Habari ID: 3472521 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/02
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatazamiwa kuakhirishwa kutokana na hofu ya kirusi cha Corona.
Habari ID: 3472513 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/27
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu amesema kuwa Iran imejitayarisha kikamilifu kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona na kwamba mahospitali yote hapa nchini yana vifaa vya kutosha vya kukabiliana na virusi hivyo.
Habari ID: 3472508 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/26
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru wananchi kwa kuufuzu kwa kiwango cha kuridhisha mtihani mkubwa wa uchaguzi na kuweza kuzima propaganda za kila upande za maadui na kutumia kwao vibaya suala hilo na akasisitiza kwamba: Taifa zima linapaswa kuwa macho na kujiweka tayari kukabiliana na njama za adui zinazolenga kutoa pigo kwa mihimili tofauti ya nchi.
Habari ID: 3472499 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/23
Imam wa Ahlul Sunna mjini Zahedan, Iran
TEHRAN (IQNA) - Imam wa Ahul Sunna katika mji wa Zahedan, kusini mashariki mwa Iran ameashiria kuenea virusi vya Corona na kusema Mtume Muhammad SAW alitoa nasaha kuhusu namna ya kukabiliana na magonjwa ambukizi ya tauni na kipindupindu.
Habari ID: 3472498 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/23
TEHRAN (IQNA)- Jildi ya 27 ya Kamusi Elezo (ensaiklopedia) ya Ulimwengu wa Kiislamu imechapishwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3472496 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/22
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, amesema, kaulimbiu ya "Mauti kwa Marekani" imetimia kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Majlisi ya 11 ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na uchaguzi mdogo wa Baraza la 5 la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Habari ID: 3472492 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/21
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo asubuhi, amepiga kura katika dakika za awali kabisa za kuanza zoezi la upigaji kura za uchaguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uchaguzi mdogo wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.
Habari ID: 3472491 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/21
TEHRAN (IQNA) - Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa, Agnès Callamard amesema Marekani ilikiuka sheria za kimataifa kwa kumuua , Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3472490 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/20
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema Marekani itazama kama ilivyozama ile meli kubwa maarufu ya Titanic.
Habari ID: 3472484 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/18
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kusimama kidete katika njia ya muqawama au mapambano na njia ya demokrasia ya kuitishwa kura ya maamuzi ili Wapalestina wenyewe waamue mustakabali wao ndilo suluhisho la kadhia ya Palestina.
Habari ID: 3472483 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/18
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amenukulu aya ya Qur'ani Tukufu kuhusu wakimbizi na akazipongeza Iran na Pakistan kutokana na ukarimu wao katika kuwapa hifadhi wakimbizi wa Afghanistan.
Habari ID: 3472482 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/18
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuendelea uungaji mkono wa Iran kwa Syria katika vita dhidi ya ugaidi.
Habari ID: 3472480 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/17
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havina faida kwa maadui na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu imevuka vikwazo vya kiwango cha juu vya Marekani.
Habari ID: 3472478 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/16
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuhusu mahudhurio makubwa ya wananchi imara wa Iran katika maandamano ya Bahman 22, na katika kuusindikiza mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwamba uthabiti mkubwa wa taifa la Iran wa kuyakabili mashinikizo makubwa na ya kinyama ya Marekani umewastaajabisha wafuatiliaji wa masuala ya kimataifa.
Habari ID: 3472474 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/15
TEHRAN (IQNA) - Marasimu ya maombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) yamefanyika Alhamisi kote nchini Iran kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa matabaka mbalimbali ya wananchi.
Habari ID: 3472469 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/14