Katika taarifa siku ya Ijumaa, Sheikh Ahmed al Tayyib amelaani pia kimywa cha jamii ya kimataifa kuhusu uchokozi wa wazi wa Israel dhidi ya Iran.
Aidha ameukosoa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kulisikuma eneo kuelekea katika vita vya pande zote huku akilaani kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu uchokozi wa Israel dhidi ya Iran. Amesema kukaa kimya kuna maana ya kuunga mkonon jinao za Israel na natija yake itakuwa ni ukosefu wa usalama duniani kote.
Taarifa hiyo imekuja baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutekeleza hujuma ya kichokozi dhidi ya Iran Ijumaa iliyopita ambapo ulilenga maeneo ya kijeshi na kiraia ya Iran. Katika kujibu, Iran inaendelea kulipiza kisasi kwa kutekeleza Operesheni Ahadi ya Kweli III kwa kulenga ngome za kijesi na kijasusi za Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
3493514