IQNA

Iran imeulazimu utawala wa Kizayuni kukubali kushindwa

23:58 - June 24, 2025
Habari ID: 3480853
IQNA-Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limetoa taarifa Jumanne na kuthibitisha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umelazimika kukubali mapatano ya usitishaji vita.

Ifuatauo ni taarifa hiyo

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu

“Hakika wale wanaosema: ‘Mola wetu ni Mwenyezi Mungu,’ kisha wakasimama imara, haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.

- Surah Al-Ahqaf, Ayah 13

Kwa taifa lenye fahari na uthabiti la Iran,

Katika kukabiliana na uchokozi wa adui Mzayuni, vjana wenu shupavu na wanaojitolea muhanga katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walitii amri ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Amiri Jeshi Mkuu. Kwa ujasiri wa kupigiwa mfano, walitoa jibu kali kwa kila kitendo cha uhasama, na kufikia kilele cha mashambulizi ya hivi karibuni kwenye kambi ya jeshi la Marekani  huko Al Udeid , Qatar, na mashambulio ya makombora yaliyofuata katika maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu (Israel).

Umakini wenu usio na kifani, hisia ya kutambua zama, Muqawama, umoja na mshikamano ulivuruga mkakati wa msingi wa adui na kutoa fursa ya kusimama kidete wa wapiganaji wa Uislamu—na nguvu ya kutisha ambayo wameikuza kwa miaka mingi ya mapambano ya kibunifu na jitihada za kudumu—kutumika kwa ufanisi katika siku kumi na mbili za vita vya umwagaji damu lakini vya busara, kujibu kila kitendo cha uchokozi kwa wakati ufaao na kwa uwiano.

Zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na  uelewa huu wa kina na wa maana na msimamo wa taifa, azimio na mapambano ya wapiganaji, na uongozi wa busara, ilikuwa ushindi na msaada kutoka kwa Mungu. Hili lilimlazimu adui kujutia matendo yake, kukubali kushindwa, na kusitisha mashambulizi yake kwa upande mmoja.

Kwa ajili hiyo, taifa kubwa na shujaa la Iran linafahamishwa kwamba, Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kupuuza kikamilifu maneno ya adui na vikiwa katika hali ya tahadhari, viko tayari kutoa jibu madhubuti na la kumfanya adhui kutokana na hatua yake yoyote ya uhasama.

Ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu tu—Mwenyezi Mungu, Mwenye hikima.

3493567/

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iran vita israel
captcha