“Umoja wenu na uwepo wenu ndiyo ulikuwa jibu kubwa zaidi kwa adui wa Kizayuni anayeua watoto,” alisema Ghalibaf katika ujumbe wake, ambao unasomeka hivi:
“Enyi watu wa Iran, wenye heshima, utu na fahari! Leo historia imefungua ukurasa mpya tena katika mitaa ya nchi hii. Kwa hatua zenu zilizojaa hamasa na imani, mmebeba miili mitukufu ya wana wa ardhi hii waliouawa shahidi, na mmeonesha kuwa Iran bado ni nchi ya watu wenye adhama.
Nainamisha kichwa changu mbele ya adhama ya uwepo wenu katika hafla ya kuwaaga makamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu , kuanzia shahidi Saeed Izadi, shahidi Gholamreza Mehrabi, hadi mashahidi Hajizadeh, Rabbani, Shadmani, Shahriari, Rashid, Kazemi, Bagheri, na Salami, waliotoa maisha yao kupinga uchokozi wa Kizayuni.
Pamoja na mashujaa hao, wanasayansi na wasomi mashuhuri waliouawa pia wameungana nao mbele ya Mwenyezi Mungu , akiwemo Dkt. Fereydoun Abbasi Davani, Dkt. Tehranchi, Dkt. Minouchehr, Dkt. Zolfaghari, Dkt. Fiqhi, Dkt. Motalebizadeh, Dkt. Asgari, Dkt. Hashemitabar, Dkt. Soleimani, Dkt. Bakuei, Dkt. Borji Kazerouni, Dkt. Sadati, na Dkt. Seddighi Saber , na kuandika ukurasa mwingine wa dhahabu katika historia ya fahari ya taifa hili.
Ninyi wananchi leo hamkubeba miili tu, bali mlijitwika pia bendera ya heshima ya Iran, na kwa mara nyingine mkadhihirisha kwamba “Labbaik ya Khamenei” ni Labbaik ya Hussein, na mkathibitisha kuwa mnathamini uongozi wa busara na ujasiri wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei.
Kwa niaba ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), ninatoa shukrani za dhati kwa kila mmoja wenu, watu wa Iran, kwa uaminifu wenu, imani, msimamo thabiti na ukuu wenu.
Katika siku hizi nyeti, umoja na uwepo wenu umekuwa jibu la dhahiri kwa adui wa Kizayuni anayeua watoto. Leo dunia imeuona umoja wa Iran; hata wale walio na tofauti za maoni nasi, walikuja pamoja katika kuilinda Iran na damu ya mashahidi.
Na tufanye ahadi na mashahidi wetu: kwamba tutaendeleza njia yao, kujenga Iran imara, huru, yenye heshima na nguvu. Na tukaahidi kuwa damu ya wapendwa wetu haitabaki ardhini bila haki.
Wasalamu Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh”
Tehran iliamka na hali ya huzuni na mshikamano, huku maelfu ya waombolezaji wakikusanyika Jumamosi kwa ajili ya mazishi ya “Mashujaa wa Nguvu ya Iran.”
Wakazi wa Tehran, wakiwa wamehamasika na roho ya Imam Hussein (AS) katika mwezi huu wa Muharram, walibeba bendera nyekundu zilizoandikwa “Labbaik Ya Hussein”, pamoja na mabango yaliyoandikwa kwa mkono yaliyojaa kauli dhidi ya Israel na Marekani. Kauli za “Maauti kwa Israel” na “Maauti kwa Amerika” zilienea katika umati.
Maafisa wengi wa ngazi za juu, wakiwemo viongozi wa mihimili mitatu ya dola, walihudhuria hafla hiyo ya mazishi.
Familia nyingi ,wakiwemo watoto na vijana , walishiriki katika msafara huo, wakionyesha uendelezaji wa maadili ya kujitolea, ushujaa, na upinzani kwa kizazi kijacho.
Utawala wa Israel ulianzisha hujuma kamili dhidi ya ardhi ya Iran mnamo Juni 13, ukishambulia maeneo ya kijeshi na ya nyuklia, na kuwaua makamanda wa ngazi za juu, wanasayansi wa nyuklia, na raia wa kawaida. Hujuma hiyo ilisababisha mashahidi 628 na kuwajeruhi zaidi ya watu 4,800.
Katika kujibu, vikosi vya jeshi la Iran vilipiga kwa makombora ya kizazi kipya yaliyolenga kwa usahihi miundombinu ya kijeshi na viwanda vya utawala wa Kizayuni.
Baada ya siku 12, utawala haramu wa Israel ulilazimika kutangaza usitishaji mapigano wa upande mmoja, kufuatia makubaliano yaliyopendekezwa na muitifaki wake mkuu, Marekani, kwa lengo la kuzuia mashambulizi zaidi kutoka kwa makombora ya Iran.
3493624