IQNA

Wairani 606 wameawa shahidi katika Siku 12 za Uvamizi wa Israel

0:15 - June 25, 2025
Habari ID: 3480854
IQNA - Waziri wa Afya wa Iran Daktari Mohammad Reza Zafarghandi amesema idadi ya waliouawa katika hujuma ya utawala wa Israel dhidi ya Iran ni 606.

Tangu kuanza kwa vita hivi vya kulazimishwa, watu 5,332 waliojeruhiwa walipokea matibabu katika vituo vya matibabu vya Waziri wa Afya, alisema Jumanne.

Saa 24 zilizopita kumeshuhudiwa mashambulizi na hujuma za kikatili zaidi za utawala wa Kizayuni tangu kuanza kwa vita hivi, ambapo watu 1,032 wamejeruhiwa na 107 wameuawa shahidi hadi leo asubuhi, amebainisha.

Vita vya uoga vya Israel dhidi ya Iran vimesababisha kuuawa shahidi kwa watu 606 hadi sasa, alisema, akiongeza kuwa asilimia 95 ya mashahidi walikufa chini ya vifusi, wakati asilimia tano tu ya waliojeruhiwa ambao walipelekwa hospitali walikufa.

Akizungumzia kujitolea mhanga kwa wafanyakazi wa afya katika mstari wa mbele wa vita hivi, Waziri wa Afya alisema: "Jana, kutokana na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni katika maeneo yanayozunguka Hospitali ya Khatam Al-Anbiya mjini Tehran, tulilazimika kuwahamisha wangonjwa ambao walikuwa katika Hospitali ya Shahid Motahari Burn, ambayo iko karibu na hospitali hii, na kuwapleka wote katika hospitali nyingine."

Aliendelea kusema kwamba “katika wiki hizi mbili za vita, tulilazimika kuhamisha wagonjwa waliokuwa hospitali tatu zilizo hatarini kuokoa maisha ya wagonjwa.

"Kulingana na uzoefu wa vita vya miaka minane (vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran na janga la coron, duru tatu za kipaumbele zilipangwa kushughulikia hali ya waliojeruhiwa katika vita, ambayo kwa bahati nzuri ilifanywa kwa njia ya kuridhisha na usimamizi mzuri wa wakuu wa vyuo vikuu vya sayansi ya matibabu na vituo vya afya vya nchi hiyo na wafanyikazi wenzake wote wa afya.

4290610

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iran vita israel
captcha