IQNA

Umoja wa Waislamu waimarika baada ya operesheni ya Iran dhidi ya Israel

5:38 - June 25, 2025
Habari ID: 3480855
IQNA - Mshikamano wa Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu umefikia kiwango kisicho na kifani kufuatia Operesheni ya Ahadi ya Kweli III dhidi ya utawala wa Israel, mwanazuoni mmoja anasema.

Haya ni kwa mujibu wa Hujjatul-Islam Hamidreza Gharibreza, mkurugenzi wa Taasisi ya Mazungumzo ya Madhehebu kuhusu Umoja, ambaye alitoa kauli hizo katika kikao cha Qom siku ya Jumatatu.

Gharibreza alikosoa mikakati ya Magharibi inayotenganisha dini na siasa. Alisema wanafikra wa Kimagharibi, wakiwa wamegundua dosari katika dini, "walizisoma na kuzitumia vibaya" - na hivyo kusababisha Mkataba wa Sykes-Picot wakati wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, ambao ulisambaratisha Milki ya Ottoman.

Alieleza kuwa makubaliano hayo yaliweka mipaka kwa misingi ya makosa ya kikabila lakini alisema migawanyiko hii ilizuiliwa na Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, ambayo yalikuza umoja wa Kiislamu.

Gharibreza aliashiria vita vya Israel vya 2006 na Hizbullah, akisisitiza kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakati huo ilisema vita hivyo viliashiria kuanza kile ilichokitaja kuwa "Mashariki mpya ya Kati." Lakini alisema vita hivyo "ingawa vilikusudia kuunda Mashariki ya Kati mpya, badala yake vilishuhudia kuongezeka kwa Mhimili wa Muqawama na makabiliano na utawala wa Kizayuni."

Ameongeza kuwa Operesheni ya Ahadi ya Kweli ya III iliibua hali ya kukataa tamaa katika utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi za Magharibi. "Waislamu duniani kote wana ndoto ya enzi mpya ya dhahabu ya Uislamu," alisema.

Alibainisha mabadiliko mawili makubwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu: kwanza, "idadi kubwa ya Masunni, wakiwemo wasomi katika nchi za Kiislamu" kuikubali itikadi ya Ushia; pili, kuibuka kwa "Ushia wa kisiasa", uliopata msukumo kutoka mapinduzi na maadili ya Ashura.

Amesema kwamba matukio haya yalichochea mawimbi ya chuki dhidi ya Iran Iranophobia na  chuki dhidi ya Mashia au Shiaphobia, iliyochochewa na madola ya Magharibi na baadhi ya serikali za Kiarabu.

Alitangaza kwamba wakati Operesheni ya Kweli ya Ahadi III ilipotekelezwa, "ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu ulipigwa na butwaa. Walipinga viongozi wao, na wimbi kubwa la uungaji mkono liliibuka kwa mgomo wa Iran dhidi ya Israeli".

Amesema operesheni hiyo imeleta "mageuzi ya kiroho na kiitikadi ambayo hayajawahi kutokea" kwa ajili ya Iran na Ushia.

"Kombora la Iran leo lina ufanisi mara mia zaidi kuliko mkutano wowote wa umoja wa Kiislamu," alisisitiza.

"Ulimwengu wa Kiarabu umebadilika baada ya kushuhudia  Iran ilivosimama kidete katika vita dhidi ya Israel. Hatimaye, ulimwengu mpana wa Kiislamu - na hasa ulimwengu wa Kiarabu - sasa uko tayari kujinasibisha na Iran."

Iran inatumia haki ya kujilinda baada ya utawala wa Israel kuanzisha hujuma ya kijeshi dhidi ya Iran tarehe 13 Juni, ikilenga maeneo ya makazi na kijeshi, na kuwaua makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia.

Vikosi vya jeshi la Iran vilianzisha Operesheni Ahadi ya Kweli III, ikilenga miundombinu ya kijeshi ya utawala huo kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora. Aidha Iran imetekeleza operesheni malaumu dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani huko Qatar na Iraq ambavyo vimekuwa vikitumiwa katika uchokozi wa Israel dhidi ya Iran.

4290466

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iran vita israel
captcha