Katika ujumbe alioutuma kwa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), Sheikh Abdul Fattah Taruti amebainisha mshikamano wake na taifa adhimu la Iran wakati huu wa kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unaendeleza mashambulizi ya kichokozi dhidi ya Iran.
Sheikh Taruti katika ujumbe wake ameomba dua ya ushindi kutoka kwa Allah kwa taifa la Iran kupitia Baraka za Qur’ani Tukufu. Akilihutubu taifa la Iran amesema: “Wamisri pamoja na viongozi wao wako pamoja nanyi, wanawaunga mkono yote ambayo mnafanya dhidi ya adui Mzayuni aliyeanzisha hujuma.”
Sheikh Taruti aidha ametangaza mshikamano na watu wa Iran katika mapambano yao dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kwa kusoma aya za Sura an-Nasr kama ilivyo katika klipu hii hapa chini.
Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha uchokozi dhidi ya Iran Juni 13 kwa kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya meneo ya kiraia na kijeshi. Makamanda wa ngazi za juu wa kijeshi pamoja na wanasayansi wa nyuklia na idadi kubwa ya raia, hasa wanawake na watoto wameuawa katika hujuma hiyo ya Israel.
Katika kujibu uchokozi huo, Iran ilianzisha operesheni yakijeshi iliyopewa jina ya Ahadi ya Kweli III, ambapo hadi sasa imevurumisha mamia ya makombora na ndege za kivita zisizo na rubani dhidi ya Israel na kulenga vituo vya kijeshi na kijasusi vya utawala huo dhalimu.
4289281