IQNA- Baraza la Maulamaa wa Kiislamu Palestina limetoa taarifa na kutangaza kufungamana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3480845 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/19
IQNA- Qari mashuhuri wa Misri, Sheikh Abdul Fattah Taruti, ametangaza kufungamana na watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3480844 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/19
IQNA- Rais wa zamani wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu, Sheikh Ahmed al Raissouni, ametoa wito kwa Waislamu duniani kote kuunga mkono Iran katika kukabiliana na hujuma ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, huku akisisitiza kuwa hakuna taifa ambalo limewaunga mkono ukombozi wa Palestina kama ilivyofanya Iran.
Habari ID: 3480843 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/19
IQNA-Kiongozi mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Mashia wa Iraq Ayatullah Sistani amelaani vikali hujuma inayoendelea ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na vitisho vyovyote dhidi ya maisha ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Habari ID: 3480842 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/19
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa la Iran litasimama kidete katika kukabiliana na vita vya kulazimishwa, kama ambavyo halitakubali amani ya kutwishwa na hivyo taifa hali halitasalimu amri.
Habari ID: 3480841 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/18
(IQNA) – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Bwana Abbas Araghchi, amefafanua kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya makombora ya Iran yalikuwa ni kitendo halali cha kujilinda, yaliyotekelezwa kujibu uchokozi wa wazi wa Israel dhidi ya maeneo ya kijeshi na ya kiraia.
Habari ID: 3480839 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/15
IQNA – Naibu Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu Iran ambaye anasimamia masuala ya Qur'ani na Itrah amelaani vitendo vya hivi karibuni vya uchokozi vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kusisitiza azma ya jumuiya ya Qur'ani nchini kufungamana na utamaduni wa muqawama (mapambano ya Kiislamu) na kuupinga utawala wa Kizayuni sambamba na kutetea maadili ya Kiislamu.
Habari ID: 3480838 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/15
IQNA-Mashambulizi ya makombora ya Iran ya jana usiku ya kulipiza kisasi jinai za Israel ni makubwa kiasi kwamba hadi hivi sasa taasisi za utawala wa Kizayuni zimeemewa na hazijui zianzie wapi.
Habari ID: 3480836 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/15
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa Vikosi vya Ulinzi vya Iran vitachukua hatua kali na kuufanya utawala wa Kizayuni wa Israel ufedheheke.
Habari ID: 3480833 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/14
IQNA-Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq amelaani vikali uchokozi wa hivi karibuni wa utawala wa Israel dhidi ya Iran, na ameihimiza jamii ya kimataifa kuzuia mashine ya vita ya utawala huo wa Kizayuni.
Habari ID: 3480830 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/13
IQNA-Katika hali ambayo, meli ya "Madleen" iliyokuwa imebeba misaada ya kibinadamu ilikuwa imekaribia Gaza, majeshi ya utawala haramu Israel yalishambulia meli hiyo katika hatua iliyotajwa kimataifa kuwa ni uharamia, na kuwateka nyara abiria wake na hivyo kuzuia misaada hiyo kufika Gaza.
Habari ID: 3480818 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/10
IQNA-Zaidi ya watu mashuhuri 300, wakiwemo waigizaji, wanamuziki na wanaharakati, wametuma barua kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, wakimtaka asitishe uungaji mkono wa Uingereza kwa Israel katika vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3480758 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/30
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuutaka usitishe hujuma na jinai zake dhidi ya Ukanda wa Gaza vinginevyo utaendelea kuandamwa na mashambulio.
Habari ID: 3480756 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/29
IQNA-Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, katika mkutano na maafisa wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani, Vatican huko mjini Rome, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa kukomesha uhalifu unaoendelea kutendwa na utawala katili wa Israel huku Gaza, na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika katika eneo hilo lililozingirwa.
Habari ID: 3480732 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/24
IQNA – Nchi wanachama wa Muungano wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) zimetoa wito wa kuwekwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Israel, huku utawala huo ukiwa unaendelea na vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3480695 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/17
IQNA – Utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia ardhi za Palestina kwa mabavu umejaribu mbinu mbalimbali kuiba hati za kale za Kiislamu.
Habari ID: 3480640 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/05
IQNA – Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kuwepo harakati za jamii ya kimataifa ili kusitisha mauaji makubwa ya kimbari ya karne hii.
Habari ID: 3480607 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/28
IQNA – Mbio za Marathon za London zilikumbwa na vurugu baada ya waandamanaji kuitaka serikali ya Uingereza kuweka vikwazo kamili vya biashara dhidi ya Israel.
Habari ID: 3480606 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/28
IQNA – Nchi kadhaa za Kiarabu zimelaani vikali kusambazwa kwa klipu iliyotengenezwa kwa kutumia Akili Mnemba (AI) na walowezi wa Kizayuni wa Israel, inayoonyesha uharibifu wa Msikiti wa Al-Aqsa ulioko katika al-Quds inayokaliwa kwa mabavu, na ujenzi wa hekalu la Kiyahudi mahali pake.
Habari ID: 3480568 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/20
IQNA – Katibu Mkuu wa Hizbullay ya Lebanon amepuuzilia mbali wazo la kuipokonya harakati hiyo, silaha zake na kusema wale wanaotoa wito wa kufanya hivyo wanahudumia ajenda ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Habari ID: 3480562 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/19