iqna

IQNA

IQNA – Watu wa Tunisia wamefanya maandamano katika mji mkuu Tunis na miji mingine siku ya Ijumaa, wakitaka kuwekwa sheria ya kuzuia uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni. 
Habari ID: 3480531    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/12

IQNA-Kamati ya Ijtihad na Fatwa ya taasisi moja ya kimataifa ya wanazuoni Kiislamu imesisitiza kuwa kuanzisha Jihad dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Isarel unaoendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza ni wajibu wa Kiislamu.
Habari ID: 3480496    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/05

Taarifa
IQNA-Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la nchini Iran (IRGC) limetoa taarifa na kutangaza kuwa kambi ya Muqawama, hususan wanamapambano shupavu na mashujaa wa Palestina, hatimaye itamaliza na kuyakatisha maisha ya aibu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakaliwa ardhi za Palestina kwa mabavu.
Habari ID: 3480490    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/04

IQNA-Takriban Wapalestina 120,000 walikusanyika kwa ajili ya Swala ya Idul Fitr katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel licha ya vikwazo vilivyowekwa na vikosi vya utawala huo dhalimu.
Habari ID: 3480476    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/31

IQNA -Majeshi ya Yemen yamelenga kwa mafanikio uwanja mmoja wa ndege wa Israel na manuwari ya Marekani yenye uwezo wa kusheheni ndege za kivita katika mashambulizi ya makombora siku ya Jumatatu.
Habari ID: 3480434    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/25

IQNA-Mkuu wa Shirika la UN la Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) ametahadharisha kwamba hatua ya utawala wa Israel kuweka mzingiro na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika Ukanda wa Gaza inapelekea eneo hilo la pwani kukaribia baakubwa la njaa.
Habari ID: 3480426    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/24

IQNA – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina Hamas ililaani mauaji ya Salah al-Badrawil yaliyofanywa na utawala katili wa Israel, ikisisitiza kuwa kwa kila shahidi, mwenge wa Muqawama unazidi kuwa mkali.
Habari ID: 3480421    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/23

Matukio ya Palestina
IQNA-Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema upayukaji na vitisho vya Trump vinavuruga makubaliano ya kusitisha mapigano kwani vinauchochea utawala wa Kizayuni wa Israel kutotekeleza wajibu wake.
Habari ID: 3480318    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/06

IQNA – Huku mwezi mtukufu wa Ramadhani ukikaribia, kumekithiri kampeni za kususia tende zinazozalishwa au kufungashwa katika maeneo ya Palestina ambayo yametekwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3480272    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/26

IQNA – Inaripotiwa kuwa utawala haramu wa Israel unazingatia kutekeleza vikwazo vipya kuhusu kuingia Waislamu katika Msikiti wa Al-Aqsa na eneo lake la karibu katika Mji wa Kale wa al-Quds (Jerusalem) kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3480266    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/25

IQNA-Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vimemkamata na kumpiga marufuku Sheikh Najeh Bakirat, kiongozi mashuhuri wa Kiislamu Palestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa ulioko jijini Al Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3480246    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/21

Jinai za Israel
IQNA – Jumla ya wanawake na watoto 90 wa Kipalestina waliachiliwa kutoka magereza ya kuogofya ya Israel mapema Jumatatu kama sehemu ya kubadilishana wafungwa iliyohusishwa na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3480083    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/20

Muqawama
IQNA – Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni umelazimika kusitisha mapigano na Harakati ya Kiislamu ya Ukombozi wa Palestina, Hamas, huko kwa sababu ya udhaifu na kukata tamaa. Hii ni moja ya heshima za mstari wa mbele wa upinzani, alisema Hujjatul-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, akihutubia mkutano wa 13 wa "Gaza; Alama ya Muqawama" jijini Tehran.
Habari ID: 3480073    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/18

Kadhia ya Palestina
IQNA-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa, kulazimika utawala wa Kizayuni kukubali kusimamisha vita na kukomesha mauaji yake ya kimbari dhidi ya wananchi wa Ghaza, ni matunda ya Muqawama (mapambano ya Kiislamu) na kusimama imara wananchi wa ukanda huo kwa zaidi ya miezi 15.
Habari ID: 3480062    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/16

Muqawama
IQNA- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) imeidhinisha pendekezo la kusimamisha mapigano kwa Ukanda wa Gaza ambayo yamefikiwa kwa upatanishi wa Misri na Qatar.
Habari ID: 3480060    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/15

Muqawama
IQNA-Jeshi la Yemen limetangaza kwamba limeilenga kwa mafanikio Wizara ya Vita ya utawala haamu wa Israel na kuitwanga kwa kombora la balestiki.
Habari ID: 3480052    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/14

Jinai za Israel
IQNA-Katika mwaka uliomalizika wa 2024, wanajeshi wa utawala wa Kiziayuni wa Israel walibomoa kikamilifu Misikiti 815 na kuharibu mingine 151 katika Ukanda wa Ghaza. Hayo yameelezwa katika ripoti iliyotolewa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini ya Palestina.
Habari ID: 3480011    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/06

Muqawama
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, kitendo cha utawala wa Israel cha kunyakua ardhi zaidi ya Syria wa hivi karibuni baada ya kuangushwa serikali ya nchi hiyo ni sehemu ya mpango wa utawala huo wa Kizayuni unaoitwa 'Israeli Kubwa'.
Habari ID: 3479924    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/20

Jinai
IQNA-Siku moja baada ya vikosi vya ulinzi vya Yemen kushambulia mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Tel Aviv kwa kombora la 'hypersonic, la Palestina 2 ndege za kivita za Marekani na Uingereza zimeshambulia maeneo kadhaa ya Harakati ya Ansarullah katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a
Habari ID: 3479914    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/17

Jinai za Israel
IQNA-Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa wingi mkubwa wa kura maazimio mawili, moja la kutaka kusitishwa kwa mapigano mara moja katika Ukanda wa Ghaza na la pili la kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uondoe marufuku yake kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi wa Palestina, UNRWA.
Habari ID: 3479893    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/12