IQNA-Ndege za kivita za Israel zimetekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya makao makuu ya harakati za upinzani za Hamas katika mji mkuu wa Qatar, Doha, katika kile vyombo vya habari vya Israel vilikitaja kama “operesheni ya mauaji ya kisiasa.”
Habari ID: 3481212 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/10
IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameulaani vikali utawala haramu wa Israel kwa kitendo chake 'haramu, cha kinyama na kinacholenga kuvuruga amani ya eneo,' baada ya utawala huo wa Kizayuni kushambulia ardhi ya Qatar na kuwaua shahidi viongozi kadhaa wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas.
Habari ID: 3481211 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/10
IQNA – Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetaja baa la njaa linaloikumba Ukanda wa Gaza kuwa ni janga lililosababishwa na binadamu, ambalo linaweza kuzuilika na kurekebishwa endapo kutakuwepo na nia ya dhati ya kisiasa.
Habari ID: 3481208 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/09
IQNA-Kiongozi wa harakati ya Ansarullah, Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi, amesisitiza kuwa watu wa Yemen wanaendelea kufuata mwenendo wa Mtume Muhammad (S.A.W) na mafundisho ya Qur’an Tukufu.
Habari ID: 3481183 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/04
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem, ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Yemen kufuatia kuuawa shahidi kwa Waziri Mkuu wa Yemen, Ahmad Ghaleb Al-Rahawi, pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali yake katika shambulio la anga la Israel lililofanyika hivi karibuni mjini Sanaa.
Habari ID: 3481169 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/01
IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Spika wa Bunge, Mohammad Baqer Qalibaf, wamelaani vikali hujuma ya hivi karibuni ya kijeshi iliyofanywa na Israel dhidi ya Yemen, ambayo imesababisha kuuawa kwa shahidi Waziri Mkuu wa Yemen na mawaziri kadhaa wa serikali ya mapinduzi ya nchi hiyo.
Habari ID: 3481163 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/31
IQNA – Mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano la Kiislamu (OIC) ulianza Jumatatu mjini Jeddah, Saudi Arabia, ambapo washiriki wamesisitiza umuhimu wa hatua ya pamoja kusaidia Gaza na Palestina.
Habari ID: 3481136 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/26
IQNA – Kamati za Upinzani za Kawaida (PRC), muungano wa makundi ya Kipalestina, zimelaani mashambulizi ya kijeshi ya utawala wa Israel yaliyolenga miundombinu nchini Yemen.
Habari ID: 3481132 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/25
IQNA- Maandamano yafanyika Uingereza kulaani mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Gaza Maandamano makubwa yamefanyika nje ya ubalozi wa utawala wa Israel mjini London, Uingereza kulaani mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481127 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/24
IQNA – Watu wa Yemen katika mkoa wa Saada wameshiriki katika maandamano ya mamilioni ya watu Ijumaa, wakionesha mshikamano wao na watu wanaodhulumiwa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481124 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/23
IQNA-Mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool, Mohamed Salah amekosoa hatua ya Muungano wa Vyama vya Soka vya Ulaya UEFA ya kumuenzi Suleiman Al-Obeid, anayejulikana kama "Pele wa Palestina," baada ya bodi inayosimamia soka ya Ulaya kutoelezea mazingira ya kifo chake wiki hii.
Habari ID: 3481065 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/10
IQNA – Shirika moja la utetezi wa haki limeshutumu agizo jipya kutoka kwa serikali ya Trump linalozuia utoaji wa misaada ya majanga kwa majimbo na miji ya Marekani inayopinga bidhaa na makampuni ya Israel yanayoshiriki katika uhalifu wa kivita, likilitaja kuwa si la kizalendo, linakiuka katiba, na ni shambulio dhidi ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.
Habari ID: 3481048 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/07
IQNA – Mkurugenzi wa Msafara wa Hijja wa Iran ameifu mshikamano wa kimataifa uliodhihirika wakati wa vita vya siku kumi na mbili vilivyoanzishwa na utawala wa Israel dhidi ya Iran, na ametilia mkazo umuhimu wa umoja wa Waislamu kuelekea Siku ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS).
Habari ID: 3481035 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/04
IQNA – Picha zilizopigwa mwishoni mwa Julai 2025 zinaonesha athari za mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran, mwezi Juni, ambapo maeneo ya makaazi ya raia yalilengwa.
Habari ID: 3481033 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/02
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon, amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani wanatekeleza jinai za kila siku, zilizo na mpangilio mahsusi, katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481023 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/31
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatعllah Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran vimeonesha kwa dhahiri uimara wa kipekee wa Jamhuri ya Kiislamu pamoja na dhamira thabiti na uwezo wake mkubwa.
Habari ID: 3481016 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/29
IQNA-Sheikh Muhammad Ahmad Hussein, Mufti Mkuu wa Al-Quds, amepigwa marufuku na utawala dhalimu wa Israel kuingia Msikiti wa Al-Aqsa ulio mjini Quds (Jerusalem) kwa muda wa wiki moja, marufuku ambayo inaweza kuongezwa
Habari ID: 3481015 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/28
IQNA-Jeshi la majini la utawala ghasibu wa Israel limeiteka meli ya misaada iliyokuwa ikielekea Ukanda wa Gaza, ikiwa na bendera ya Uingereza, katika harakati za kuvunja mzingiro mkali wa eneo hilo unaoendelea tangu mwaka 2007.
Habari ID: 3481010 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/27
IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yameshindwa kutimiza malengo waliyojiwekea, huku akisisitiza kwamba taifa hilo litaendelea kusonga mbele kwa kasi zaidi katika nyanja za kijeshi na kielimu kwa azma iliyo imara.
Habari ID: 3481003 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/26
IQNA-Kiongozi mkuu Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, ameelezea masikitiko yake makubwa kuhusu hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, hususan baa la njaa linalozidi kushika kasi, na kutoa wito kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za haraka kukomesha janga hili la kusikitisha.
Habari ID: 3481002 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/26