iqna

IQNA

Kuhiji kwa mara ya kwanza ni ndoto iliyotimia kwa Abdi Mohammad, Mwislamu kutoka Kenya ambaye amekuwa akiuza viungo vya chakula kwa muda wa miaka 15 ili aweze kuchanga pesa za kumuwezesha kutimiza faradhi ya Hija katika mji mtakatifu wa Makkah.
Habari ID: 3366740    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/23

Zaidi ya maulamaa na maimamu 300 wa Kiislamu Somalia, Kenya, Tanzania, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametangaza Fatwa ya kupambana na kundi la kigaidi la al-Shabab na itikadi yenye misimamo mikali ya Uwahhabi.
Habari ID: 3353847    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/30

Nchini Kenya Jumuiya ya Mashekhe Waislamu Nairobi NMC wameanzisha msafara wa kuhubiri dhidi ugaidi na misimamo mikali miongoni mwa vijana Waislamu.
Habari ID: 3353707    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/29

Mufti wa Tunisia Sheikh Hamda Saeed amewaomba radhi Watunisia baada ya kubaini kuwa alifanya kosa kwa kutangaza mapema siku kuu ya Idul Ftir.
Habari ID: 3330378    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/20

Kamati ya kuutafuta mwezi mwandamo katika Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza kuwa, Siku kuu ya Idul Fitr itaadhimishwa kesho Jumamosi nchini Iran na kwa msingi huo Ijumaa ya leo ni siku ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini.
Habari ID: 3328911    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/17

Wazazi Waislamu nchini Kenya wamekosoa kitendo cha uongozi wa shule mbili cha kuwalazimisha wanafunzi wa Kiislamu kuingia makanisani kwa ibada.
Habari ID: 3322404    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/02

Jumuiya na taasisi mbalimbali za kimataifa na kiraia zimeendelea kulaani mauaji yaliyofanywa Alkhamisi iliyopita na kundi la kigaidi la al Shabab dhidi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya.
Habari ID: 3099045    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/04/06

Mjumbe katika Baraza la Kaunti ya mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya amekosoa uamuzi wa Mahakama Kuu kuwapiga marufuku wanafunzi Waislamu katika Kaunti ya Isiolo kuvaa Hijabu.
Habari ID: 2968360    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/12

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maafa makubwa yanayofanywa na makundi ya kigaidi kama lile la Boko Haram yanaathiri na kuumiza sana dhamira za wanadamu kote dunia.
Habari ID: 2771315    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/27

Waislamu nchini Kenya wanataka vyombo vya habari nchini humo vifanye mabadiliko ya kimsingi kuhusu namna vinavyo tangaza habari kuhusu ugaidi na kuonya kuwa mfumo wa sasa usio wa kitaalamu wa kutangaza habari ni chanzo cha chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Habari ID: 2617613    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/11

Waislamu nchini Kenya wamelalamikia vikali hatua ya serikali ya nchi hiyo kufunga misikiti kadhaa katika Kaunti ya Mombasa.
Habari ID: 1476305    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/23

Mahakama moja ya Kenya imetoa uamuzi wa kupiga marufuku vazi la Hijabu katika shule moja nchini humo jambo ambalo limewakasirisha sana Waislamu wakiwemo wazazi na wanazuoni wa Kiislamu ambao wameitaja hukumu hiyo kuwa ni hatua nyuma katika uhuru wa kuabudu nchini humo.
Habari ID: 1455483    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/09/29

Banki ya KCB (Kenya Commercial Bank) nchini Kenya imetangaza kuwa itaanzisha rasmi mfumo kamili wa Kiislamu katika huduma za banki mwezi wa Agosti huku ikipanga kueneza huduma hiyo katika eneo lote la Afrika Mashariki.
Habari ID: 1434697    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/31

Baadhi ya Waislamu katika nchi za Iraq, Uturuki, Qatar, Misri, Saudi Arabia na Bahrain leo wanasherehekea sikukuu ya Idul Fitr baada ya kutangazwa rasmi mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika nchi hizo.
Habari ID: 1434339    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/28

Viongozi wa Kiislamu nchini Kenya wamewataka raia wa nchi hiyo kuwa na umoja na mshikamano. Viongozi hao wamekutaja kudumishwa umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi kuwa ni jambo muhimu la lenye udharura.
Habari ID: 1396701    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/04/19

Mashindano ya Qur’ani nchini Kenya yameingia wiki yake ya pili kwa kufanyika awamu ya mchujo katika Masjid Kambi eneo la Kibra katika mji mkuu, Nairobi.
Habari ID: 1390167    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/03/31

Shirika Kubwa la Bima (re-insurance au bima mara ya pili) ya Kiislamu linatazamiwa kuanzishwa Kenya baadaye mwaka huu kwa lengo la kutoa huduma kwa mashirika ya bima ya Kiislamu ijulikanayo kama Takaful nchini humo.
Habari ID: 1374704    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/02/13