hijabu - Ukurasa 3

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Liberia inayoongozwa na Rais George Weah imechukua hatua ya aina yake kuruhusu kuwaruhusu wanafunzi wa kike Waislamu wake kuvaa Hijabu wakiwa chuoni wakati wa kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3475161    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/24

TEHRAN (IQNA)- Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameonya kuwa mpango wa hasimu wake katika uchaguzi wa rais, Marine Le Pen wa kupiga marufuku hijabu katika maeneo ya umma unaweza kuibua vita ndani nchini humo.
Habari ID: 3475150    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/21

TEHRAN (IQNA)- Siku kadhaa baada ya shule za jimbo la Karanatka la kusini mwa India kuwapiga marufuku wanafunzi wanawake Waislamu kuvaa vazi la staha la Kiislamu la Hijabu, mahakama ya nchi hiyo imeidhinisha rasmi uamuzi huo wa kibaguzi.
Habari ID: 3475046    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/03/15

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu Kiislamu (WFPIST) ametoa wito kwa viongozi wa India na viongozi wa kitamaduni, kisiasa, wasomi na vyombo vya habari kusaidia kulinda haki za Waislamu wa nchi hiyo.
Habari ID: 3474987    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/28

TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya watu kutoka dini zote walikusanyika mjini Johannesburg siku ya Ijumaa kulaani ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na vitisho vya unyanyasaji dhidi ya Waislamu katika baadhi ya maeneo ya India.
Habari ID: 3474979    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/26

TEHRAN (IQNA)- Wataalamu wa haki za Umoja wa Mataifa wametaka kukomeshwa kwa mashambulizi ya mtandaoni "ya kuchukiza dhidi ya wanawake na ya kimadhehebu" dhidi ya mwanahabari Muislamu nchini India, wakiomba mamlaka kuchunguza unyanyasaji huo.
Habari ID: 3474966    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/23

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA)- Mwanamke mmoja Muislamu ameuhujumiwa akiwa ndani ya treni mjini London ambapo Hijabu yake imevutwa na mtu anayeaminikwa kuwa ni mwenye chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3474960    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/22

TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi wenye majina ya Kiislamu Ufaransa wanabaguliwa wakati wanapowasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu nchini humo.
Habari ID: 3474943    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/18

TEHRAN (IQNA)- Huku mzozo wa Hijabu ukiendelea kutokota katika jimbo la Karnataka nchini India, wanawake Waislamu wameandamana katika mji wa Ludhiana, jimboni Punjab kuunga mkono haki ya kuvaa Hijabu.
Habari ID: 3474924    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/13

TEHRAN (IQNA)- Mchezaji nyota wa Manchester United, Paul Pogba aliingia kwenye mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi na kusambaza video yenye kuwatetea wanawake Waislamu India wanaovaa Hijabu kufuatia mzozo unaoendelea kuhusu Hijab katika Jimbo la Karnataka nchini India.
Habari ID: 3474914    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/10

TEHRAN (IQNA)- Klipu iliyowekwa kwenye mtandao wa Twitter ikimuonyesha mwanafunzi Muislamu aliyevaa hijabu akibughudhiwa kwa maneno na genge la wahindu wenye misimamo ya kufurutu mpaka katika chuo kimoja cha jimbo la Karnataka nchini India, imezusha moto wa hasira na kuzidisha malalamiko ya kupinga marufuku ya uvaaji hijabu iliyowekwa katika taasisi za elimu za jimbo hilo.
Habari ID: 3474910    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/09

TEHRAN (IQNA)- Katiba ya Nigeria inaruhusu wanawake wa Kiislamu kuvaa Hijabu kulingana na mafundisho ya imani yao, waziri wa elimu wa nchi hiyo ya Kiafrika alisema.
Habari ID: 3474903    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/07

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania kimeandaa maonyesho ya Hijabu kwa ushirikiano na Taasisi ya Pink Hijab.
Habari ID: 3474897    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/06

TEHRAN (IQNA)- Baraza la Seneti la Ufaransa limepiga kura na kuidhnisha sheria inayopiga marufuku wanawake Waislamu kuvaa vazi la stara na heshima la Hijabu katika mashindano ya michezo.
Habari ID: 3474830    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/20

TEHRAN (IQNA)- Mfanya biashara mwanamke Muislamu Mjamaica ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kutekeleza sera ya kutowabagua wanawake Waislamu maeneo ya kazi na vituo vya elimu sambamba na kulinda haki zao.
Habari ID: 3474822    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/18

TEHRAN (IQNA)- Ubelgiji imeondoa marufuku ya uvaaji vazi la stara ya mwanamke wa Kiislamu Hijabu iliyokuwa imewekwa kwa wale wanaoingia katika mahakama za nchi hiyo.
Habari ID: 3474677    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/15

TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau imetangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya sheria ya jimbo la Quebec ambayo imepelekea mwalimu mmoja Muislamu ahamishwe kazi kwa sababu tu alikuwa amevaa Hijabu.
Habari ID: 3474665    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/11

TEHRAN (IQNA)- Wanafuzni Waislamu katika Chuo Kikuu cha Kyambogo mjini Kampala nchini Uganda wanataka chuo hicho kiwaajiri maafisa usalama wanawake wanawake ambao watakua na jukumu la kuwapekua wanafunzi wa kike.
Habari ID: 3474654    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/08

TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Nigeria wamemtaka wazili wa elimu nchini humo Adamu Adamu aingilie kati kuzuia kusumbuliwa wasicana Waislamu wanaochagua kuvaa Hijabu shuleni.
Habari ID: 3474646    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/06

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimekosoa uamuzi wa shule moja Uhispania kupiga marufuku vazi la Hijabu na kutaja kitendo hicho kuwa ni ubaguzi.
Habari ID: 3474523    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/06