IQNA

Umoja wa Waislamu

Rais wa Iran ahimiza Umoja kati ya Waislamu

19:04 - September 16, 2022
Habari ID: 3475791
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi kwa mara nyingine tena

"Kama vile Ahlul-Bayt (AS) ambao walikuwa alama za umoja, Waislamu wanapaswa kuwa na umoja na kukabiliana na wale wanaopinga Uislamu na kuua Waislamu," Raisi alisema siku ya Alhamisi alipokuwa akiwahutubia waumini katika Msikiti wa Ahlul-Bayt Rasuul Allah huko Samarkand nchini Uzbekistan.

Huku akitoa salamu za rambirambi kutokana msimu huu wa kukumbuka  kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), pia alizungumzia masuala tofauti ya Arbaeen.

Rais wa Iran alikuwa katika  nchi ya Asia ya kati kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ambao umefanyika Ijumaa.

Iran daima imekuwa ikisisitiza umoja katika ulimwengu wa Kiislamu. Hayati Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini alianzisha Wiki ya Umoja wa Kiislamu katika muongo 1980.

Wiki hiyo inakuja kati ya siku ya 17 ya Rabi al-Awwal ambayo inaaminika na Waislamu wa Shia kuwa ni siku  ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (SAW), na siku ya 12 ya mwezi huo ambayo Waislamu wa Sunni wanaitakidi kama siku ya kuzaliwa kwa Mtume wa mwisho.

Kila mwaka kunafanyika hafla inayoitwa Mkutano wa Umoja wa Kiislamu nchini Iran kuashiria umoja huu.

3480506

captcha