IQNA

Harakati za Kiislamu

Mwanasiasa wa Malaysia: Dira ya Mtume Muhammad (SAW) ni dira ya Umma wa Kiislamu

22:55 - October 13, 2024
Habari ID: 3479588
IQNA - Mwanasiasa wa Malaysia amesisitiza kuhusu umuhimu wa kufuata Sira ya Mtukufu Mtume Muammad (SAW) kwa Umma wa Kiislamu ili kufikia umoja.

Akizungumza na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), Abdul Hadi Awang, Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Malaysia (Parti Islam Se-Malaysia), alisema Sira ya Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu lazima iwe dira kwa Umma wa Kiislamu na ni hati ambayo Waislamu wote wanapaswa kufuata.
Kwa kufuata Sira hii, Waislamu wanaweza kuweka kando tofauti zao na kuungana dhidi ya maadui, alisema.
Mtume (SAW) daima alijitahidi kueneza udugu miongoni mwa Waislamu na waumini na hivyo ndivyo Waislamu, ambao ni wafuasi wake, wanapaswa pia kufanya, alisema.
Ameongeza kuwa, Umma wa Kiislamu una jukumu lililoanza baada ya kufariki Mtume (SAW) na halitaisha hadi Siku ya Kiyama na jukumu hilo ni kujitahidi kuwa mfano wa kuigwa duniani.
Awang ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, pia alisema kuleta mifarakano baina ya Waislamu ni njama iliyopangwa na wakoloni ili kuudhoofisha Umma wa Kiislamu kwa vile hawataki Uislamu kuenea  na kuitawala dunia.
Uislamu ndio itikadi pekee inayookoa na ina uwezo wa kuzuia kuporomoka kwa ubinadamu na kuporomoka kwa maadili mema, alisema.
Aya za Quran zinatuambia kwamba ghilba na njama za maadui dhidi ya Uislamu hazina mwisho, alisema, akisisitiza haja ya kuimarisha umoja dhidi ya njama hizi.
Katika maelezo yake ameashiria suala la Palestina na kusema kuwepo utawala wa Kizayuni katika ardhi ya Kiislamu ya Palestina ni Haramu.
Awang ameongeza kuwa, kukaliwa kwa mabavu Palestina sio tu kunyakua ardhi bali ni unyakuzi na ukoloni wa kifikra.
Suala la Palestina halihusiani tu na Waarabu, bali ni suala la ulimwengu wote wa Kiislamu, amesisitiza.
Ni haki ya Waislamu na wajibu wao wa kidini kuitawala ardhi ya Palestina, amebaini.
Chama cha Kiislamu cha Malaysia kilianzishwa katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia mwaka 1951.
Wakiwa wamevutiwa wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 nchini Iran, viongozi wa chama hicho walitangaza kuanzishwa kwa serikali ya Kiislamu kama moja ya malengo yao.

3490249

Habari zinazohusiana
captcha