IQNA

Misikiti 803 Mumbai, India yapata idhini ya kutumia vipaza sauti

12:01 - May 05, 2022
Habari ID: 3475208
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Polisi katika mji wa Mumbai nchini India imetoa idhini kwa misikitini 803 kutumia vipaza sauti kwa ajili ya adhana.

Kamishna wa polisi mjini humo Sanjay Pandey alitangaza Jumanne kuwa amepokea maombi 1,144 kutoka misikiti ya mji huo na hatimaye ametoa idhini kwa misikiti 803 kutumia vipaza sauti.

Misikiti hiyo imetakuwa kufuata maagizo ya Mahakama Kuu na Bodi ya Uchafuzi wa Mazingira ya Maharashtra (MPCB) katika utumizi wa vipaza sauti.

Hii ni mara  ya kwanza kwa idadi kubwa ya misikiti kuomba kutumia vipaza Saudi kwa ajili ya adhana. Maombi ya kutumia vipaza sauti wakati wa adhana Msikiti yalianza baada ya chama cha chenye misimamo mikali cha Maharashtra Navnirman Sena kutaka serikali iondoe vipaza sauti misikitini.

Karibu asilimia 72 ya misikiti kote Mumbai imeacha kutumia vipaza sauti wakati wa Sala y Alfajiri na inafuata maagizo ya kimazingira ya kupunguza kiwango cha sauti.

Misikiti imetakiwa ifuate sheria na uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu vipaza sauti. 

Katika miaka ya karibuni, serikali ya waziri mkuu wa India Narendra Modi imewawekea mibinyo na vizuizi vikubwa Waislamu wa nchi hiyo. Sera ya serikali ya New Delhi ya kuwakandamiza Waislamu na kuwanyima haki zao imewashajiisha Wahindu wenye chuki kutumia fursa ya uungaji mkono ya chama tawala chenye misimamo mikali na ya utaifa cha BJP, kufanya vitendo vya mauaji na kumwaga damu za Waislamu wasio na hatia wa nchi hiyo.

3478766

Kishikizo: india ، adhana ، waislamu ، bjp
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :