IQNA

Pakistan yaitaka jamii ya kimataifa kuiwajibisha India kuhusu haki Waislamu

15:37 - February 24, 2022
Habari ID: 3474971
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Pakistan imeitaka jamii ya kimataifa, hususan Umoja wa Mataifa na mashirika husika ya kimataifa ya haki za binadamu, kuiwajibisha India kutokana na kukithiri ukiukaji wake wa haki za binadamu dhidi ya walio wachache, hasa Waislamu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, katika taarifa yake Jumatano, ilisema kwamba India lazima pia ilazimishwe kusitisha "ugaidi wake unaofadhiliwa na serikali katika Jammu na Kashmir zinazokaliwa kinyume cha sheria na India", kuondoa mzingiro wa kijeshi katika eneo hilo na kuwaacha Wakashmiri watumie haki yao ya kujitegemea na hayo yafanyika  kulingana na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa.

Kauli hiyo ilitolewa wakati wa maadhimisho ya miaka ya pili ya Ghasia za Delhi 2020 na kumbukumbu yam waka wa  31 wa ubakaji mkubwa wa wanawake wa Kashmiri katika vijiji vya Kunan na Poshpura vya Jammu na Kashmir mnamo 1991.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesema Ghasia za Delhi 2020 "ni moja ya dhihirisho mbaya zaidi la kampeni ya kimfumo ya India ya kubagua na kudhalilisha utu wa jamii ya Waislamu.

"Miito ya kuchukiza ya 'kuwapiga risasi wasaliti' iliyitolewa na viongozi wakuu wa chama tawala BJP wakati wa maandamano dhidi ya Sheria ya Marekebisho ya Uraia ya kibaguzi zilifichua kina cha chuki na uhasama ulioidhinishwa na serikali nchini India dhidi ya Waislamu," ilisema.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa "ya kutisha vile vile ni kumbukumbu mbaya ya ubakaji wa 1991 wakati askari wa India waliwabaka bila huruma zaidi ya wanawake 40 wa Kashmir katika vijiji vya Kunan na Poshpura vya IIOJK. Tangu wakati huo, wahasiriwa wa ubakaji mkubwa wa Kunan-Poshpura wanangojea haki."

3477937/

Habari zinazohusiana
Kishikizo: pakistan india waislamu bjp
captcha