IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Msukosuko baada ya hoteli kufuta Kongamano la Kundi la Waislamu la Marekani

15:53 - January 10, 2024
Habari ID: 3478178
IQNA - Shirikisho la Waislamu wa Florida Kusin nchini Marekani lilikuwa limepanga kufanya mkutano wake wa kila mwaka katika Hoteli ya Fort Lauderdale Marriott Coral Springs na Kituo cha Mikutano wikendi hii, lakini hoteli hiyo imekataa ukumbi wake utumike wiki moja kabla ya tukio.

Shirikisho hilo, ambalo linawakilisha misikiti yote katika eneo hilo na linafanya kazi ya kukuza umoja na uungwaji mkono miongoni mwa jamii za Kiislamu na zisizo za Kiislamu, lilisema uamuzi wa hoteli hiyo ulitokana na "tuhuma za kibaguzi, zisizo na msingi" kutoka kwa mwanasiasa wa zamani ambaye alidai kundi hilo linaunga mkono ugaidi.

"Hatukufikiri ubaguzi wa rangi ungetawala katika Florida Kusini kwa njia hii," alisema Jalal Shehadah, mwanachama wa shirikisho na mjumbe wa zamani wa Baraza la Ushauri la Waislamu na Wayahudi, CBS News iliripoti Jumanne.

Meneja mkuu wa hoteli hiyo, Mark C. Cherry, alidai katika barua pepe kwamba hoteli hiyo imebaini kuwa kuna hatari kubwa kwa usalama wa wageni wa hoteli hiyo, wafanyakazi na jamii iwapo kongamano hilo litafanyika. Alisema hoteli hiyo imefanya uamuzi wa kutoandaa hafla hiyo baada ya kutafakari kwa kina masuala hayo.

Kughairiwa huko kumekuja baada ya Joe Kaufman, ambaye aligombea ubunge mara tatu bila mafanikio, kuandika makala mtandaoni ambayo inadai kuwa baadhi ya wazungumzaji katika mkutano huo wataeneza chuki na itikadi kali. Pia alianzisha ombi lililokusanya maelfu ya saini za kupiga marufuku mkutano huo.

Kaufman na wengine wanne walikutana na Cherry wiki iliyopita ili kuelezea wasiwasi wao. Shehadah alisema hakualikwa kwenye mkutano na alifahamu tu kuhusu kughairiwa wakati Cherry alipompigia simu baadaye.

Shehada alisema shirikisho hilo linatafuta eneo jipya la mkutano huo unaotarajiwa kuanza Ijumaa na kumalizika Jumamosi. Alisema anahisi kuwa kughairishwa kwa hoteli hiyo sio tu kwamba kunarudisha nyuma tukio hilo, bali pia ni pigo kwa utu na haki za jamii ya Kiislamu.

3486756

Habari zinazohusiana
Kishikizo: marekani waislamu cair
captcha