IQNA

Wafanyaziyara ya Arbaeen wakiwa njiani kuelekea Karbala

11:04 - October 05, 2020
Habari ID: 3473232
TEHRAN (IQNA) - Waislamu, aghalabu wakiwa ni wa madhehebu ya Shia, kutoka kila kona za Iraq wako katika matembezi ya wiki kadhaa ya kuelekea katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya maadhimisho ya Arobaini ya Iman Hussein AS.

Matembezi ya siku ya Arobaini hufanyika kila mwaka wiki kadhaa kabla tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria. Siku ya Arbaeen huadhimishwa baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbalamwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

 
captcha