Haya ni kwa mujibu wa Wizara ya Wakfu Gaza ambayo pia imesema katika ripoti yake kwamba mabomu na makombora ya utawala wa Kizayuni pia yameharibu kwa kiasi misikiti mingine 200 ya Gaza.
Taarifa hiyo imebaini kuwa asilimia 60 ya misikiti katika eneo hilo la Palestina imepata uharibifu wa kiwango kikubwa katika mashambulizi ya Israel.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala ghasibu wa Israel pia umelenga makaburi 60 katika Ukanda wa Gaza ambapo askari wake wamefukua na kuiba miili ya zaidi ya mashahidi 1,000 Wapalestina.
Wizara ya Wakfu Gaza pia haijasalimika, ripoti hiyo ilisema, huku majengo 15 ya wizara hiyo, yakiwemo makao makuu yake makuu, makao makuu ya Redio ya Qur'ani, idara ya wakfu huko Khan Yunis na kituo cha makumbusho na makavazi kuharibiwa kabisa katika mashambulizi ya Israel.
Pia, wafanyakazi 91 wa Wizara ya Wakfu Gaza wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel hadi sasa.
Kulingana na sheria za kimataifa, kushambulia misikiti na maeneo mengine ya ibada na turathi kunachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita.
3488381