IQNA

Diplomasia

Rais wa Iran amwambia Sultan wa Oman: Umoja wa Waislamu utamaliza jinai za Wazayuni

20:55 - October 17, 2024
Habari ID: 3479608
IQNA- Rais wa Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Iwapo nchi za Kiislamu zitaungana zenyewe, utawala wa Kizayuni wa Israel hatathubutu kufanya jinai kirahisi na Marekani na nchi za Magharibi pia hazitaunga mkono utawala huo."

Rais Pezeshkian ameyasema hayo jana alipozungumza kwa simu na Sultan wa Oman, Haitham bin Tariq, ambapo alisisitiza kuhusu kuimarika kwa udugu baina ya nchi za Kiislamu za eneo la Asia Magharibi pamoja ulazima wa kutilia maanani mafunzo ya Kiislamu yanayoegemea Sira ya Mtume Muhammad (SAW), kuwa ni masuala ya lazima wakati huu.
Rais wa Iran pia ametaka kushinikizwa waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni ili kusitisha moto wa vita na jinai za mauaji ya kimbari zinazotekelezwa na utawala huo.
Rais Pezeshkian pia amepongeza misimamo thabiti ya Oman dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza na Lebanon. Pezeshkian aidha amesisitiza kushinikizwa waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni ili kukomesha moto wa mauaji na jinai za utawala huo ghasibu.  
Rais Masoud Pezeshkian ametaja kuimarisha uhusiano kati ya Iran na Oman kuwa kati ya vipaumbele vya sera kuu za Jamhuri ya Kislamu katika kustawisha uhusiano na majirani zake na kuongeza kuwa kuimarisha uhusiano wa kirafiki na wa karibu kati ya nchi za eneo hili pamoja na kupanua ushirikiano wa kikanda ni dhamana ya kuwa na mtazamo na lugha ya pamoja kwa ajili ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali za kikanda kama jukwaa la maendeleo ya pamoja ya nchi na kukuza ustawi, amani na utulivu wa watu wetu."
Katika mazungumzo hayo ya simu, Sultan wa Oman amesema kuwa kuunga mkono haki za wananchi madhulumu wa Gaza na Lebanon ni katika vipaumbele na daghadagha kuu za nchi yake na kwamba Oman siku zote inasisitiza kuwa uungaji mkono endelevu wa nchi za Magharibi kwa jinai za Israel haukubaliki na hauwezi kuhalalishwa kwa namna yoyote ile. 
4242782

captcha