IQNA

Matembezi ya Arbaeen

Silaha Zilizopatikana Karbala, watu wenye itikadi kali Wakamatwa Najaf

21:56 - September 13, 2022
Habari ID: 3475775
TEHRAN (IQNA) – Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (PMU) kimegundi maroketi katika mji mtakatifu wa Karbala wakati siku ya Arbaeen inapokaribia huku idadi kubwa ya wafanyaziara wakiwa wamekusanyika kwenye mji huo mtakatifu.

PMU,ambayo pia inajulikana kama Hashd al-Sha'abi, ilisema kitengo  chake cha kutegua mabomu  kilifanikiwa kupata na kugundua silaha hizo.

Timu za PMU zilidokezewa na wananchi walioripoti vifaa vya ajabu vilivyoachwa nyuma ya Moukeb (mahali pa kupumzikia kwa wafanyaziara wa Arbaeen).

Kwa ushirikiano wa Kikosi cha Ulinzi wa Raia wa Iraq, makombora na maroketi yaliwasilishwa kwa idara ya ujasusi ya Karbala.

PMU pia ilisema imeimarisha uwepo wake katika maeneo kadhaa nchini ili kuhakikisha usalama na usalama wa mahujaji wa Arbaeen.

Wakati huo huo, vyombo vya usalama vya kitaifa vya Iraq vilitangaza kuwa vikosi vyake vimewakamata watu 8 wenye misimamo mikali ya kidini katika mkoa wa Najaf.

Ilisema wao ni wanachama wa kundi la kidini lenye misimamo mikali na walitishia usalama na amani. Katika habari nyingine, kamanda wa polisi wa shirikisho la Iraq alisema vikosi vya polisi vimetumwa Baghdad, Najaf na Karbala ili kuwahudumia na kuhakikisha usalama wa wafanyaziara wakati wa matembezi  ya Arbaeen.

Maadhimisho ya maombolezo ya Arbaeen (Arubaini) ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.

Inaadhimisha siku ya 40 baada ya Ashura, kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS). Arbaeen ya mwaka huu itaangukia Septemba 17.

Kila mwaka umati mkubwa wa Waislamu hasa Mashia na hata wasiokuwa Waislamu humiminika Karbala, kuliko Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo.

Wafanyaziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri njia ndefu kwa miguu hadi mji huo mtakatifu.

4085127

captcha