IQNA

' Karbala ni njia ya kuelekea Al-Aqsa'Kauli mbiu ya Arobaini ya 2024

19:12 - June 23, 2024
Habari ID: 3479003
IQNA - Afisa mmoja anasema kauli mbiu ya maandamano ya mwaka huu ya Arbaien ilichukuliwa kwa kuzingatia ukandamizaji wa kikatili unaoendelea wa Israel dhidi ya watu wa Palestina.

Kila mwaka, kauli mbiu ya Arbaini huchaguliwa kwa uangalifu kulingana na hali na mahitaji yaliyopo huku kundi la wanaharakati wa ndani na nje na wataalamu wakishauriwa katika mchakato huo, Hujat-Al-Islam Hamid Ahmadi, mkuu wa kamati ya kitamaduni ya Makao Makuu ya Arbaini ya Iran, aliiambia. IQNA siku ya Jumapili.

Mwaka huu, utaratibu wa uteuzi ulianza mapema ili kuruhusu watu wanaotayarisha bidhaa za kitamaduni na mipango zinazohusiana na Arbaini kuanza shughuli zao mapema.

Wakati wa mwezi wa Aprili na Mei mwaka huu, vikao vya mapitio ya kauli mbiu ya Arbaini vilifanyika na maafisa wa Iraq, kulingana na ripoti za Ahmadi. 

Kuna mwamko unaoongezeka duniani kote kuhusu ukatili mkubwa unaofanywa na utawala wa Israel dhidi ya watu wa Palestina huko Ukanda wa Gaza, alisema.

Kwa kuzingatia jukumu la Arobaini kama vuguvugu la "kupambana na ukandamizaji na uchokozi", mijadala ilijikita katika kuingiza suala la Palestina huko Ukanda wa Gaza katika harakati zake za kitamaduni, aliongeza.

Kauli mbiu "Karbala Tariq al-Aqsa" (Karbala ni Njia ya Kuelekea al-Aqsa) ilichaguliwa kuashiria ukombozi na uhuru wa Quds Tukufu Ahmadi alisisitiza.

Chaguo hili linaonyesha uhusiano kati ya Karbala, vuguvugu la Ashura, na njia ya kuelekea uhuru wa watu wa Palestina, alisema.

Matamshi hayo yanakuja wakati Wapalestina zaidi ya 37,000 wameuawa katika hujuma ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda Gaza tangu Oktoba mwaka jana. Wengi wa waathirika ni wanawake na watoto.

Vile vile suala la Arobaini pia linajulikana kama Ziyara ya Arobaini, ambayo ina maana ya kutembelewa kwa kaburi la Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq, ambapo mwili wake umezikwa. Ziyara ni tendo la kuhiji na kujitolea katika Uislamu wa Shia.

Arobaini ni miongoni mwa safari kubwa zaidi za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia kutoka mataifa mbalimbali wakitembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Umbali unaweza kuanzia km 80  hadi  km 500  au zaidi, kulingana na mahali pa kuanzia.

Arobaini ya mwaka huu inatarajiwa kuwa mnamo Agosti 25, kulingana na mwangaza wa mwezi.

348885

 

 

Kishikizo: karbala iraq arbaeen
captcha