Hafla hiyo ilianza rasmi saa nne unusu leo lakini watu kutoka mbali na karibu walifika kwenye sherehe hiyo kuanzia saa kumi na moja asubuhi na wakati milango ya Uwanja wa Sala wa Imam Khomeini (RA) ilifunguliwa kwa ajili ya kuwakakribisha waumini waliofika katika hafla ya Sayyid wa Muqawama (Sayyid Hassan Nasrallah). Waumini waliofika wamebainisha kuchukizwa na jinai za kikatili za utawala mashuhuri wa Kizayuni huko Gaza na Lebanon.
Katika hafla hiyo inayofanyika kufuatia kuuawa shahidi mshika bendera ya muqawama na uhuru wa Quds na Palestina, Seyyed Hassan Nasrallah na Kiongozi wa Hamas Ismail Haniya pamoja na mashahidi wenzao, na katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa Operesheni ya Kimbunga cha Al- Aqsa ya wapiganaji wa harakati za muqawama (mapambano ya Kiislamu ya Palestina), Sala ya Ijumaa wiki hii mjini Tehran, Oktoba 4, itaswalishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Hafla hiyo ya Khitma na Swala ya Ijumaa imeanza kwa usomaji wa aya za Qur’ani Tukufu na Qari Mohammad Hossein Saidian.
Baadaye, Ahmed Babaei, mshairi mwanamapinduzi, alisoma mashairi ya kuomboleza kwa ajili ya Sayyid Hasan Nasrallah.
Baada ya hapo, Hossein Al-Akarf, msoma mashairi wa Bahrain, alisoma tungo za nafasi ya mujahid katika Njia ya Allah Allah, Sayyid Hassan Nasrallah.
Kisha, Haj Mehdi Rasuuli, mtunzaji wa Ahlul-Bayt (pbuh), akasoma mashairi yanayoelezea hadhi ya juu ya Shahidi Seyyed Hassan Nasrallah. Hafla hiyo imeendelea kwa kusomwa mashairi na aya za Qur’ani Tukufu kabla ya Kiongozi Muadhamu wa Mapindzi ya Kiislamu kuanza hotuba za Swala ya Ijumaa.
4240473