IQNA

Harakati za Qur'ani

Misri yahuisha qiraa maarufu za Qur’ani kwenye mitandao ya kijamii

21:00 - December 15, 2024
Habari ID: 3479901
IQNA -Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu nchini Misri limetangaza kuachiliwa kwa usomaji nadra wa Qur'ani kutoka enzi ya dhahabu ya sanaa ya Qur'ani ya Misri kwenye kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Mpango huu ambao ni wa kwanza kutekelezwa na baraza hilo unalenga kusambaza klipo  zinazopendwa na Waislamu duniani kote.

Qiraa hizo ni sehemu ya harakati mpya za Qur’ani kwenye majukwaa rasmi ya mitandao ya kijamii ya Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu na Wizara ya Wakfu za Kidini ya Misri.

Juhudi hizi, kulingana na ripoti hiyo, zinalenga kutumia teknolojia ya kisasa kufikia hadhira ya kimataifa kwa sauti nzuri za maqari mashuhuri wa Misri.

Qiraa hizo ni pamoja na sauti za wasomaji mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kama vile Mahmoud Khalil al-Hussary, Abdul Basit Abdul Samad, Mustafa Ismail, na Mahmoud Ali al-Banna. Wasomaji hawa, wanaosifika kwa mitindo yao ya kipekee, wamekuwa jukumu muhimu kuitangaza Misri duniani kote kama kitovu cha Qiraa ya Qur’ani Tukufu.

Baraza hilo linasemekana lina akiba kubwa ya qiraa Qur'ani kupitia rekodi za wasomaji mashuhuri wa Misri katika miaka iliyopita.

3491049

Kishikizo: qurani tukufu misri qari
captcha