IQNA

Msikiti Mkuu wa Makka wapokea waumini Milioni 4 katika sku Moja 

17:40 - March 28, 2025
Habari ID: 3480456
IQNA – Msikiti Mkuu wa Makka,  Masjid al Haram, eneo takatifu zaidi katika Uislamu, uliwapokea waumini, wakiwemo Mahujaji wa Hija ndogo ya Umrah,zaidi ya milioni 4 kwa siku moja katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Kwa mujibu wa Mamlaka Kuu ya Kushughulikia Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu, takriban waumini milioni 3.4 walikusanyika kwa ajili ya swala kwenye msikiti huo katika siku ya 26 ya Ramadhani, ambao walijumuisha Mahujaji 800,000. Takwimu hizo zilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Ghazi Al Shahrani. 

Takwimu za mahudhurio zilionyesha kwamba takriban watu 703,000 walihudhuria swala ya Fajr, 614,300 swala ya Adhuhuri, 643,900 swala ya Alasiri, 740,100 katika swala ya Magharibi na idadi hiyo hiyo katika swala ya Ishaa.

Ramadhani, inayotarajiwa kumalizika Jumamosi, kwa kawaida huandamana na kukithirishwa ibada. Idadi kubwa ya Waislamu kutoka Saudi Arabia na nje ya nchi hutembelea Msikiti Mkuu wa Makka katika kipindi hiki kwa ajili ya swala na kutekeleza Umrah.

Mamlaka za Saudi azimechukua hatua za kusimamia idadi kubwa ya wageni, ikiwa ni pamoja na kuteua milango maalum kwa mahujaji. Juhudi za kuhakikisha usalama na utulivu zimeongezwa kadri idadi ya wageni inavyoongezeka, hasa katika siku za mwisho za Ramadhani. 

3492518/

captcha