IQNA

Mufti Mkuu wa Oman Aikosoa OIC kwa Kunyamaza Kuhusu Uhalifu wa Israel

13:24 - February 03, 2026
Habari ID: 3481885
IQNA — Mufti Mkuu wa Oman amekosoa vikali ukimya na kutochukua hatua kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) pamoja na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kuhusu uhalifu unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Katika taarifa yake, Sheikh Ahmed Al-Khalili amesema kuwa uhalifu wa majeshi vamizi dhidi ya wananchi wa Palestina unaendelea licha ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Ameeleza kuwa mashambulizi hayo yanafanyika ilhali makubaliano hayo yalitiwa saini kwa usimamizi wa baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu, jambo linalozua swali zito: Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu iko wapi? Jumuiya ya Nchi za Kiarabu iko wapi? Na iko wapi dhamira na hamasa ya Umma wa Kiislamu, ilhali hakuna hatua yoyote inayochukuliwa?

Akirejea kuendelea kwa hujuma na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza na maeneo mengine ya Palestina, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano, Mufti huyo ameonesha masikitiko yake makubwa juu ya kushindwa kwa nchi hizo kulaani waziwazi uonevu unaoendelea.

Amesisitiza kuwa ukimya huo hauishii kwa nchi zilizohusika katika kusimamia makubaliano pekee, bali umeenea katika ulimwengu mzima wa Kiarabu na Kiislamu, hali inayozidisha maswali ya msingi: “OIC iko wapi? Jumuiya ya Nchi za Kiarabu iko wapi? Na iko wapi ghayra ya Kiislamu?”

Habari inayohusiana:

Akinukuu maneno ya Mtume Muhammad (SAW), Mufti Mkuu wa Oman amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila Muislamu kusimama imara na kupambana na dhulma hii kwa nguvu na uwezo wote aliojaaliwa.

4331960/

Habari zinazohusiana
captcha