
Mashindano haya yatatangazwa mubashara kupitia mtandao huo katika mwezi mzima wa Ramadhani, huku washiriki wakitakiwa kutuma majina kamili pamoja na nchi wanayoishi, kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na kuwasilisha uthibitisho wa umri, sambamba na kutuma namba za mawasiliano na utambulisho wa Skype kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika kwa njia ya mtandao.
Ili kushiriki katika hatua ya awali, washiriki wanatakiwa kutuma faili ya sauti wakitilawa moja kati ya kurasa maalum za Qur’ani kupitia WhatsApp.
Hatua ya kwanza ya mashindano, ambayo ilianza mwanzoni mwa Ramadhani 2024, iliundwa kwa raundi tatu kila moja ikidumu siku nane, ambapo jumla ya washiriki 96 walishindana kwa usiku 24 na 24 bora wakaingia fainali.
Waandalizi wamesisitiza kuwa “Wa Rattil” ni mashindano ya kwanza ya kimataifa katika ulimwengu wa Kiislamu yaliyotengwa mahsusi kwa sanaa ya Tarteel, yakilenga kuonyesha ubora wa tilawa ya Qur’ani na kuhamasisha ushiriki na Qur’ani Tukufu miongoni mwa jamii mbalimbali.
TV ya Thaqalayn ilizinduliwa kwa lugha ya Kiarabu katika Ramadhani 1430 Hijria (2008 Miladiya), ni chombo cha kidini, Qur’ani na kitamaduni kinachozingatia masuala ya ulimwengu wa Kiislamu na Umma wa Kiislamu kwa kutayarisha na kutangaza vipindi mbalimbali, vikilenga kufufua na kueneza utamaduni na elimu za Kiislamu, pamoja na kuimarisha familia ya Kiislamu ya kisasa kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.
3495973