IQNA

"Tuko Katika Ahadi": Kaulimbiu Kuu ya Matembezi  ya Arbaeen    

23:38 - May 06, 2025
Habari ID: 3480646
IQNA-Iran imetangaza kaulimbiu rasmi ya matembezi adhimu ya ya Arbaeen mwaka 1447 (2025), ni Inna Ala Al-Ahd" (Tuko Katika Ahadi") ili kuonyesha uaminifu kwa maadili ya Imam Hussein (AS). 

Kaulimbiu hii ilitangazwa katika kikao cha 86 cha Kamati ya Utamaduni na Elimu ya Arbaeen, kilichofanyika Mei 6. Maafisa wakuu wa Iran, wakiwemo wawakilishi wa masuala ya Hija na Ziyara, walihudhuria. 

Kwa mujibu wa Hujjatul Islam Hamid Ahmadi, mwenyekiti wa kamati hiyo, kaulimbiu huchaguliwa kila mwaka ili kuonyesha roho ya Ashura na kuwasilisha ujumbe wake kwa muktadha wa sasa wa kikanda na kimataifa. 

Kaulimbiu ya mwaka huu ilipitishwa baada ya mashauriano ya miezi kadhaa na tathmini ya wataalam, huku ikihusiana na historia ya harakati ya Ashura na ibada ya Arbaeen. 

Mohammad-Taqi Baqeri, Katibu wa Kamati Kuu ya Arbaeen, alieleza kuwa lengo kuu la kamati ni kuimarisha utamaduni wa kiroho na kuhakikisha wanaoshiriki katika matembezi na Ziyara ya Arbaeen nchini Iraq wanapata huduma bora, ikiwa ni pamoja na usafiri, bima, na huduma za ardhini. 

Arbaeen huadhimisha siku ya 40 baada ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), katika Vita vya Karbala mwaka 61 Hijria. Kila mwaka, mamilioni ya watu hasa Waislamu wa madhehebu ya Shia husafiri kwenda Karbala kuadhimisha tukio hilo, likiwa moja ya makusanyiko makubwa zaidi ya kidini duniani.  

3492961

captcha