IQNA

Msomi: Qur’ani imeitaja Hija kuwa 'Bendera ya Uislamu'

20:42 - May 17, 2025
Habari ID: 3480698
IQNA – Ibada ya Hija, inayofanywa kila mwaka, inatajwa katika Qur’an kama bendera ya Uislamu, kulingana na maelezo ya mwanazuoni wa Kiislamu kutoka Iran.

Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Seyed Reza Akrami alieleza kuwa Hija inapaswa kutambulika kama chuo kikuu, maonyesho, kituo cha mafunzo, utafiti na warsha.

Katika Qur’an kuna sura inayoitwa Surah Al-Hajj, inayotambulisha ibada ya Hija kama bendera ya Uislamu, ikitangazwa kamamwito wa Ibrahimu, unaotoka kwenye kina cha roho yake, ukialika ulimwengu kutekeleza Hija

Ameisitiza kuwa ibada ya Hija inabeba manufaa makubwa kwa jamii ya Kiislamu na hata kwa wanadamu kwa ujumla.

"Mahujaji, wakiwa wamevaa vazi la ihram, hufanya udhu, tawafu, na Sa’i baina ya Safa na Marwah pamoja, wakitekeleza ibada za Hija. Kutokana na mtazamo huu, Hija ni njia ya kujisafisha, kujenga jamii, kukuza mshikamano na kuimarisha mahusiano ndani ya Umma wa Kiislamu," aliongeza.

Akirejelea Aya ya 28 ya Surah Al-Hajj: "Ili washuhudie manufaa yao…", alisema kuwa ni mwito kwa mataifa na watu wa dunia kuungana katika ibada ya Hija ili kutambua maslahi yao wenyewe, mshikamano, maelewano, uhusiano, umoja na uhai wa kiroho.

Alieleza kuwa faida hizi si za ulimwengu huu tu, bali pia zina thamani kubwa ya kiroho kwa maisha ya akhera.

Alipotakiwa kuelezea jinsi Hija inaweza kutumiwa kupinga juhudi za kusahaulisha suala la Palestina na pia kuwazindia watu kuhusuuhalifu wa utawala wa Kizayuni, Hujjatul Islam Akrami amesema kuwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (RA) alipendekeza kufanyika kwa ibada ya bar’aat min-al-mushrikeen (kujitenga na kujibari na washirikina) katika Hija, ili kuonyesha wazi urafiki na marafiki wa Mungu na uadui na maadui wa Mungu.

Ibada hii ya kujitenga na washirikina ni sehemu ya Hija ili kuwafanya madhalimu watambue kuwa wanachukiwa, na wenye kudhulumiwa waelewe kuwa wanapewa msaada wa kudumu. Hili linafanyika kupitia kauli mbiu, uelewa na matendo ili mahujaji waweze kutambua na kutekeleza Hajj kwa uelewa wa kina.

3493116

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija qurani tukufu
captcha