IQNA

Waislamu Marekani

Wanawake wa Kiislamu wavuliwa Hijabu maafisa wa polisi Marekani

14:39 - August 23, 2024
Habari ID: 3479317
IQNA - Polisi wa Marekani mjini New York (NYPD) walirarua hijabu za wanawake wengi wa Kiislamu waliokuwa wakiandamana nje ya mkutano wa kukusanya fedha wa Kamati ya Kitaifa ya chama cha Democrat wiki iliyopita.

Mnamo Agosti 14, waandamanaji walikusanyika katika hafla ya Kamala Harris, iliyohudhuriwa na Meya wa New York Eric Adams na wanasiasa wengine. Hali ilizidi kuwa mbaya wakati waandamanaji, waliokuwa kando ya barabara, waliripotiwa kushambuliwa na maafisa wa NYPD.

Ripoti zinaonyesha kuwa maafisa walirarua hijabu za waandamanaji wanawake wa Kiislamu, kulingana na Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR).

Shajnin Howlader, mmoja wa waandamanaji walioripotiwa kuvuliwa hijabu, alieleza tukio hilo: “Nilifika nyumbani usiku ule nikiwa nimepatwa na kiwewe kabisa, mwili wangu ukiwa unauma kwa kusukumwa na kushikwa na polisi, nilikuwa na maumivu kichwani baada ya nywele zangu kuvutwa na polisi. Nimeshindwa kulala ipasavyo tangu wakati huo kwani kila wakati nakumbuka hijabu yangu ilivyovutwa wa nguvu. Sijawahi kukutana na kitu kama hicho.  Nataka haki kwa ajili yangu na wengine waliokuwa wamevaa hijabu ambao walikumbwa na udhalilishaji usiku huo.”

Tawi la New York la Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR-NY) limekashifu vikali ukatili wa polisi.

Katika taarifa yake, mwanasheria wa CAIR-NY Christina John alisema: "Matendo ya NYPD kwa wanawake wa Kiislamu waliovaa hijab ni ya kuchukiza kwa sababu ni ukatili wa kimwili, ukiukwaji wa uhuru wa kimwili, na ukiukwaji wa haki za kidini. Unyanyasaji kama huo unaofanywa na wasimamizi wa sheria ulimzuia Shajnin na wanawake wengine wasitumie haki zao kwa mujibu wa katiba."

3489616

Habari zinazohusiana
Kishikizo: marekani waislamu cair
captcha