Chuo Kikuu cha Al-Azhar, mojawapo ya taasisi mashuhuri zaidi ya Kisunni katika ulimwengu wa Kiislamu, kilitoa tamko kali siku ya Alhamisi kikilaani ziara hiyo, na kuitaja kama usaliti wa maadili ya Kiislamu na utu wa kibinadamu.
Kundi hilo la wageni liliripotiwa kuwa na watu kutoka Ufaransa, Uingereza, na Italia, ambao walidai kwamba walikuwa wakipeleka “ujumbe wa amani” na “kukuza mazungumzo baina ya dini.”
Katika tamko lake, Al-Azhar imewakosoa 'Mashekhe' hao kwa kupuuza “mauaji ya kimbari, ukatili usio na kifani na kuendelea kwa mauaji ya watu wasio Palestina kwa zaidi ya miezi ishirini.”
Tamko hilo liliendelea kueleza kuwa ujumbe wa 'Mashekhe' hao “hauwakilishi Uislamu wala Waislamu” na likatoa onyo kuhusu watu ambao “wameuza dhamira zao za kidini na maadili yao kwa ajili ya maslahi binafsi au ya kisiasa.”
Ukosoaji pia ulitolewa kutoka barani Ulaya. Baraza la Maimamu wa Ulaya lilijitenga wazi 'Mashekhe' hao, likisema kuwa ujumbe huo hauhusiani na taasisi yoyote ya Kiislamu inayotambulika miongoni mwa Waislamu wa Ulaya.
Tulishtushwa na taarifa za vyombo vya habari kuhusu ziara ya maimamu wanaojiita hivyo kwa utawala ghasibu (Israel) na kukutana kwao na viongozi wa kivita wa utawala huo dhalimu, Baraza limesema, likiitaja ziara hiyo kuwa “ya kichokozi” na inayohusiana na “ajenda zenye mashaka.”
Ujumbe huo, ambao ulikutana na rais wa utawala wa Kizayuni, Isaac Herzog, mapema wiki hii, unatarajiwa kubaki katika ardhi hizo zilizokaliwa kwa mabavu kwa siku kadhaa, ukifanya mikutano na viongozi wa kisiasa, kijeshi, na kidini. Pia walitembelea Msikiti Mtakatifu wa Al-Aqsa katika mji wa Al-Quds Mashariki unaokaliwa kwa mabavu.
Ziara hiyo iliandaliwa na ELNET, shirika lisilo la kiserikali la Ulaya linalolenga kukuza mahusiano kati ya Ulaya na utawala haramu wa Israel.
Ziara hiyo imefanyika wakati ambapo tangu kuanza kwa uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 2023, zaidi ya Wapalestina 57,700—wengi wao wakiwa wanawake na watoto—wameuawa. Eneo hilo pia linakabiliwa na baa la njaa kutokana na Israel kuzuia kwa makusudi kuingia kwa chakula na misaada ya kibinadamu.
Licha ya kuanzishwa kwa taasisi iitwayo Gaza Humanitarian Fund kwa ushirikiano na Marekani, kwa madai ya kusambaza chakula, Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa takriban Wapalestina 800 wameuawa na wanajeshi wa Israel wakati wakisubiri misaada katika vituo hivyo vya usambazaji.
3493801