Sherehe ya ufungaji, iliyoendeshwa ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makkah au Masjid al Haram siku ya Jumatano, ilihitimisha siku sita za mashindano ya mwisho ya kusoma, kuhifadhi na kufasiri Qur’ani.
Toleo la mwaka huu limewashirikisha mashindano washiriki 179 kutoka mataifa 128, wakiwania katika vitengo vitano, huku zawadi zikifikia jumla ya Riyal za Kisaudia milioni 4. Majaji wa kimataifa walisimamia mashindano hayo wakisaidiwa na mfumo mpya wa kielektroniki ili kuongeza usahihi na uadilifu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Saudi, washindi katika kila kundi ni kama ifuatavyo:
Mohammad Adam Mohammad (Chad)
Anas bin Majid Al-Hazmi (Saudi Arabia)
Sanusi Bukhari Idris (Nigeria)
Mansour bin Muteb Al-Harbi (Saudi Arabia)
Abdulwadud bin Sudayrah (Algeria)
Ibrahim Khairuddin Mohammad (Ethiopia)
Mohammad Damaj Al-Shuwaigh (Yemen)
Mohammad Mohammad Kussi (Chad)
Badr Jang (Senegal)
Mohammad Amin Hassan (Marekani)
Mohammad Kamal Mansi (Palestina)
Nasr Abdul-Majeed Amer (Misri)
Bayu Wibisono (Indonesia)
Tahir Batil (Kisiwa cha Réunion)
Yusuf Hassan Othman (Somalia)
Boubacar Diko (Mali)
Anu Intarat (Thailand)
Salahuddin Hussam Zani (Ureno)
Chang Wana Su (Myanmar)
Abdulrahman Abdulmunim (Bosnia na Herzegovina)
Anis Shala (Kosovo)
Viongozi waliohutubu pia waliwapongeza majaji pamoja kwa usimamizi bora..
Katika kipindi chote cha mashindano, washiriki wa fainali walisoma kwa utulivu na taadhima ndani ya Msikiti Mtukufu, katika vikao vya asubuhi na jioni.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudi (SPA), zawadi zote zilifikia Riyal milioni 4, na kila mshiriki alipewa posho maalumu.
Mashindano haya yanatajwa miongoni mwa matukio ya kimataifa yenye heshima kubwa zaidi ya Qur’ani Tukufu, yakiwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa Waislamu na Kitabu Kitukufu pamoja na kukuza maadili ya wastani na uvumilivu.
Aidha, mwaka huu programu iliambatana na ziara za kitamaduni mjini Madina kwa washiriki, ili kuunganisha ibada na historia ya Kiislamu.
/3494344