IQNA

Aya za Qur’ani, kaligrafia ya Kiarabu na ramani za nchi katika kazi za Msanii wa Mosul

15:42 - August 22, 2025
Habari ID: 3481119
IQNA-Jannat Adnan Ahmed, msanii mashuhuri wa khatt kaligrafia kutoka Mosul, Iraq, na anayeishi New Zealand, anajulikana kwa kazi zake za kipekee zinazochanganya aya za Qur’ani na ramani za nchi za Kiarabu.

Alizaliwa mwaka 1965 na tangu utotoni alivutiwa na kaligrafia kutokana na mapenzi ya baba yake kwa sanaa hii tukufu. Kufikia umri wa miaka kumi tayari alikuwa amepata vyeti, na akawa msanii mdogo zaidi wa kike duniani katika khatt.

Alijifunza mikononi mwa mabingwa kama Yusuf Dhanun, na mwaka 1975 alipata leseni rasmi kutoka kwa Hamed al-Amadi, kisha akathibitishwa pia na Sayyid Ibrahim wa Cairo. Ustadi wake mkubwa upo katika mitindo ya Thuluth, Thuluth Jalli na Tughri, na ana uwezo wa nadra wa kuandika kwa mikono yote miwili kwa wakati mmoja.

Quranic Verses, Arabic Calligraphy, and Maps of Countries in Works of Calligrapher from Mosul

Mradi wake “Jiografia ya Mistari” ni ujumbe wa mapenzi na mshikamano wa Kiarabu, ambapo ramani za nchi huchorwa kwa aya maalumu za Qur’an. Katika ramani ya Iraq aliandika dua ya Nabii Ayyub (AS) akiomba rehema; Syria aliandika aya ya subira na pepo; Palestina akaweka dua ya uthabiti na ushindi; na Qatar akaandika maneno ya uhuru na imani.

Kwa Jannat, ubora wa sanaa si kanuni pekee bali ni urari wa maneno na maumbo ya kimaono. Kupitia khatt wake, anatuma ujumbe wa umoja, amani na mapenzi ya Uislamu.

Ndoto yake ni kurejea Mosul, kujenga tena misikiti na masoko yake ya kale, na kuyapamba kwa khatt kama urithi wa imani na tamaduni.

Quranic Verses, Arabic Calligraphy, and Maps of Countries in Works of Calligrapher from Mosul

Quranic Verses, Arabic Calligraphy, and Maps of Countries in Works of Calligrapher from Mosul

3494333

captcha