IQNA

Kikao cha Khatmul Qur’an chafanyika Oman jijini Salalah

14:01 - December 30, 2025
Habari ID: 3481736
IQNA – Hafla ya Khatm Qur’an imefanyika katika mji wa Salalah, Oman, ikihusisha washiriki 110 waliokuwa wamehifadhi Qur’ani Tukufu.

Khatmul Qur’an humaanisha kusoma Qur’ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho katika kikao kimoja, jambo linaloashiria ukamilifu wa utii na ibada. Hafla hii iliandaliwa na Kituo cha Qur’ani cha Salalah, kinachohusiana na Jumuiya ya Qur’ani ya Oman, chini ya usimamizi wa Ahmed bin Mohsen Al-Ghassani, Meya wa Dhofar, na ikiwa sehemu ya mradi wa kituo hicho wa mwaka 2025.

Shughuli hii ilishuhudia ushiriki mpana wa wanafunzi waliorejelea walichokihifadhi kutoka Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa ukamilifu au kwa sehemu. Jumla ya wahifadhi Qur’ani 110 wa kiume na wa kike walihudhuria, na wakagawanywa katika makundi mbalimbali: waliokamilisha Qur’ani nzima (6), waliosoma sura 20 (6), waliosoma sura 15 (5), waliosoma sura 10 (12), waliosoma  sura 5 (41), na waliosoma sura 2 (40).

Raed bin Awad Balkhair, Mkurugenzi wa Kituo cha Qur’ani Salalah, alisema kuwa hafla hiyo ilihudhuriwa na makundi mbalimbali ya jamii ya Oman, wakiwemo wanaume na wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea, waliobobea katika usomaji wa Qur’ani kwa wepesi na ustadi.

Aliongeza kuwa umuhimu wa tukio hili ni kuimarisha ufahamu wa hadhi ya Qur’ani Tukufu na kuhimiza umakini kwa Neno la Wahyi kupitia kuhifadhi, kusoma na kutafakari aya zake. Aidha, lengo lilikuwa ni kukagua na kuimarisha hifadhi ya Qur’ani miongoni mwa washiriki, kugundua vipaji vipya vya Qur’ani, kuwaandaa na kuwahimiza kushiriki mashindano ya kitaifa na kimataifa ya Qur’ani, pamoja na kuunda roho ya hamasa, mashindano na kujiamini kwa washiriki.

Mji wa Salalah, makao makuu ya mkoa wa Dhofar, upo katika pwani ya kusini ya Oman, na ni kitovu cha kiutamaduni na kiroho cha eneo hilo.

3495889

Kishikizo: oman qurani tukufu
captcha