IQNA

Jinai za Israel zaendelea, Wapalestina 21 wapoteza maisha katika baridi kali Gaza

10:30 - January 13, 2026
Habari ID: 3481797
IQNA – Tangu kuanza kwa vita vya kikatili vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, angalau Wapalestina 21 wamefariki katika eneo hilo kutokana na baridi kali na ukosefu wa vifaa vya kujihifadhi na kupashia joto, hali ambayo imesababisha na hatua ya Israel kuzuia misaada kufika eneo hilo.

Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina iliripoti Jumatatu kwamba watu 21, wakiwemo watoto 18, wamepoteza maisha kutokana na baridi kali katika mahema ya wakimbizi tangu mwanzo wa vita hadi Januari 11, 2026.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa janga kubwa la kibinadamu linaendelea kutanda Gaza, likichochewa na sera zisizo za kibinadamu za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Soma zaidi

“Dhima kamili na ya moja kwa moja ya uhalifu huu na athari zake za maafa inabebwa na utawala wa Kizayuni, sambamba na sera ya mauaji ya taratibu, njaa na kuwafurusha watu wa Gaza,” taarifa hiyo ilisomeka.

Ofisi hiyo ilitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, Umoja wa Mataifa, pamoja na taasisi za kibinadamu na za kisheria kuingilia kati kwa dharura, kwa kutoa maeneo salama ya hifadhi, kuruhusu upatikanaji usio na vikwazo ndani ya Gaza, na kuokoa maisha yaliyosalia.

3496045
Kishikizo: gaza jinai za israel
captcha