
Imesisitizwa kuwa kongamano hilo, ambalo limebeba kaulimbiu ya “Haki za Binadamu na Heshima ya Mwanadamu katika Mafundisho ya Kivilizishaji ya Ahlul-Bayt (AS), kwa mkazo maalum juu ya mafundisho ya Imam Ridha (AS)”, litafanyika katika mji mtukufu wa Mashhad nchini Iran mwezi Juni.
Kwa msingi huo, wito umetolewa kwa wataalamu na wanataaluma kushiriki kwa kuwasilisha tafiti zao.
Kongamano hili, linaloandaliwa kwa juhudi za Taasisi ya Kisayansi na Kitamaduni ya Astan Quds kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Tehran, linatarajiwa kuchambua mada pana zinazogusa utu wa mwanadamu, uadilifu wa kijamii, maadili, falsafa na mifumo ya uongozi. Kwa mtazamo wa taaluma mbalimbali na fikra za ustaarabu, mkusanyiko huu unalenga kufafanua namna mafundisho ya Imam Ridha (AS) yanavyoweza kuwa dira ya mizani, maadili ya msingi, na thamani za kiutu katika nyanja za kielimu na kiufikra.
Mada za kongamano hili zimegawanywa katika maeneo sita ya msingi: fitri na kimungu, kifalsafa, kijamii, kisiasa, kiraia, na kiakhlaqi. Wanazuoni, wanafikra na wanaharakati wa kijamii wanakaribishwa kushiriki na kuchangia katika kuwasilisha mfano wa ustaarabu unaolenga kuimarisha hekima ya kimaadili, uadilifu wa kijamii, maisha yenye upeo wa juu wa kiroho, pamoja na mazungumzo ya tamaduni mbalimbali.
Watafiti na wahadhiri wanaweza kupakia muhtasari wa makala zao, usio na chini ya maneno 1,000, hadi mapema mwezi Machi kupitia tovuti rasmi ya kongamano, gcir.razavi.ir, baada ya kujisajili.
Kongamano hili linachukuliwa kuwa miongoni mwa matukio muhimu ya kielimu yanayochunguza kwa kina mafundisho ya Imam Ridha (AS), haki za binadamu kwa mtazamo wa Kiislamu, na falsafa ya kivilizishaji ya Ahlul-Bayt (AS).
Habari inayohusiana:
Historia yake inarudi zaidi ya miongo minne nyuma, na katika matoleo yaliyopita, kwa ushiriki wa wanazuoni wa ndani na nje ya nchi, ujumbe muhimu wa kielimu na kitamaduni uliwasilishwa na kujadiliwa kwa kina.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano, tembelea: https://gcir.razavi.ir/en
4329916