
Saudi Arabia ilipokea waumini wa ibada ya Umrah wapataoo milioni 19.5 kutoka mataifa mbalimbali mwaka 2025, na kufanikisha kiwango cha kuridhika kwa huduma kilichozidi asilimia 90, Shirika la Habari la Saudi (SPA) liliripoti, likinukuu Kituo cha Kitaifa cha Upimaji wa Utendaji wa Taasisi za Umma (Adaa).
Takwimu hizi za kihistoria zinaakisi maendeleo ya haraka na ya kina katika huduma zinazotolewa kwa waumini wanaotekeleza ibada ya Umrah.
Mpango wa Kuboresha Huduma kwa Mahujaji ulieleza kuwa maboresho hayo yamehusisha misimu yote miwili ya Hija na Umrah.
Mpango huo pia uliripoti viwango vya kuridhika vya asilimia 91 miongoni mwa mahujaji wa Hija na asilimia 94 kwa washiriki wa Umrah, jambo linaloonyesha ubora wa mipango na utekelezaji wa shughuli, pamoja na mshikamano wa taasisi zaidi ya 60 zilizoshirikiana kwa uwiano mmoja kutoa huduma jumuishi.
Zaidi ya hayo, mpango huo ulisisitiza kuwa mafanikio haya ni mwendelezo wa heshima ya kihistoria ambayo Ufalme unajivunia katika kuhudumia Misikiti Miwili Mitukufu na wageni wake.
Habari inayohusiana:
Ilielezwa kuwa kuhudumia mahujaji na watendaji wa Umrah ni kipaumbele cha juu kabisa, na kwamba rasilimali zote zinaelekezwa katika kuboresha ubora wa huduma na kuimarisha utayari wa mifumo ya huduma mwaka hadi mwaka.
/3496278