IQNA

Kituo cha Qur’ani cha Wanawake Chafunguliwa Bahrain

13:09 - February 12, 2026
Habari ID: 3481924
IQNA – Kituo cha Sheikha Hessa Bint Ali Al Khalifa cha Kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Kufundisha Sayansi za Qur’ani kimefunguliwa rasmi kwa ajili ya wanawake katika eneo la Al‑Bustain, mkoa wa Muharraq, nchini Bahrain.

Kituo hiki kimeanzishwa kwa lengo la kutoa mfumo jumuishi wa kielimu unaohudumia Qur’ani Tukufu na kuimarisha nafasi ya elimu ya Kiislamu miongoni mwa wanawake na wasichana.

Uzinduzi wa kituo hicho ulifanywa na Luluah Bint Khalifa Bin Salman Al Khalifa, rais wa heshima wa Jumuiya ya Hisani ya Noor, ambayo inaunga mkono shughuli za Qur’ani na elimu ya dini.

Programu za kituo hiki zinajumuisha: ufundishaji wa tajwidi na qira’a sahihi, kufundisha mitindo saba ya qira’a (Qira’at Sab‘a), marekebisho ya usomaji wa Qur’ani, na hifdh ya Qur’ani Tukufu kwa wanawake, pamoja na masomo ya fiqhi na elimu za dini.

Aidha, kituo kinatekeleza programu maalumu ya watoto ijulikanayo kama “Iqra Wartaq – Soma na Panda Daraja”, inayowalenga watoto kuanzia umri wa miaka minne.

Programu hizi zinatekelezwa kwa mujibu wa mkabala wa kielimu na kielimu-dini wa kituo hicho, kwa lengo la kulea vizazi vinavyomudu kusoma Qur’ani kwa usahihi, vinavyofahamu hukumu za Qur’ani, na vinavyoshikamana na mafundisho ya Kitabu Kitukufu katika maisha yao ya kila siku.

Habari inayohusiana:

Kwa mujibu wa Hanan Saif bin Arabi, mkuu wa kamati ya vyombo vya habari na mahusiano ya umma ya Jumuiya ya Hisani ya Noor, msaada na uangalizi wa uongozi wa kituo hiki umechukua nafasi muhimu katika kuendeleza shughuli za Qur’ani na kazi za kheri katika jamii.

captcha