IQNA

Saudia kusambaza nakala milioni 2.2 za Qur'ani duniani katika Mwezi wa Ramadhani

15:11 - February 16, 2026
Habari ID: 3481945
IQNA – Ufalme wa Saudi Arabia umeanzisha mpango wake wa kila mwaka wa Mwezi wa Ramadhani katika ngazi ya kimataifa, unaojumuisha ugawaji wa nakala milioni 2.2 za Qur'ani Tukufu.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu, Da‘wah na Mwongozo wa Saudi Arabia, Sheikh Abdullatif Al‑Sheikh, amezindua rasmi mpango wa Ramadhani wa Mlinzi wa Misikiti Miwili Mitukufu kwa mwaka 1447 Hijria, katika hafla iliyofanyika mjini Riyadh siku ya Jumapili.

Mipango hiyo inajumuisha kuandaa iftar na kusambaza tende kwa Waislamu katika nchi 120 duniani, ikiwa ni juhudi ya kuimarisha mshikamano na kusaidiana katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mpango huu utasambaza jumla ya tani 1,000 za misaada mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la tani 300 ikilinganishwa na mwaka uliopita—na utafikisha msaada huo katika nchi 120, zikiwemo nchi 18 mpya zilizoingizwa kwa mara ya kwanza.

Aidha, mpango huo unajumuisha ugawaji wa Misahafu (nakala za Qur'ani) milioni 2.2 , pamoja na tarjuma zake katika lugha mbalimbali, kwa lengo la kueneza ujumbe wa Qur'ani na kuimarisha uhusiano wa Waislamu na Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Habari inayohusiana:

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sheikh Abdullatif Al‑Sheikh alisisitiza kuwa wizara yake imekusanya na kuhamasisha rasilimali zote za kibinadamu na kiutawala ili kuhakikisha mipango hiyo inawafikia walengwa kwa ufanisi, heshima na wakati unaofaa, hususan katika mwezi wa baraka wa Ramadhani.

3496433

captcha