
Hili liko katika fremu ya mradi unaolenga kujenga upya utu wa binadamu kiroho na kimaadili kupitia Qurani Tukufu, baada ya miaka zaidi ya miwili na nusu ya mauaji, kufukuzwa makwao, njaa na kunyimwa mahitaji ya msingi.
Kwa mujibu wa Palestine Online, katika kona moja ya shule hiyo, iliyoko ndani ya moja ya misikiti ambayo imebomoka kwa nusu huko Khan Yunis, wasichana wadogo wameketi wakiwa wameshika nakala za Qur'ani mikononi mwao, wakisoma kwa sauti ya chini na ya unyenyekevu.
Wengi wao wamepoteza nyumba na wapendwa wao, lakini katika duara hizi za hifdhu na kusoma Qur'ani wamepata pahali pa kutulia panapowapa chembe ya utulivu walioupoteza.
Huda al-Farra, mwanafunzi na mshiriki wa shule hiyo, anasema kuwa vita viliharibu nyumba ambayo ilichukua miaka mingi kujengwa na kuvunja kabisa maisha yao.
“Tulihamishwa na kuishi kwenye mahema, lakini vita havikuweza kuuangamiza moyo wetu; tukakimbilia kwenye Qur'ani ili kuinuka tena na kupumua pumzi mpya katika wakati mgumu kama huu,” anasema kwa sauti yenye uchungu.
Akitaja kuwa shule hiyo ya Qur'ani imekuwa uwanja wa wanafunzi kushindana katika kuhifadhi Qur'ani na kujipatia elimu ya dini baada ya kushuhudia matukio ya kuuawa shahidi wapendwa wao na kufukuzwa makwao, alisisitiza kuwa kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu kume wapa nguvu ya kusubiri na kustahimili.
“Tumekuta ndani ya Qur'ani kitu cha kuishikilia ili kuinuka tena na kuendelea na maisha yetu licha ya kila kitu.”
Rami al-Shakra, Mkuu wa Kituo cha Hifdhu na Sayansi za Qur'ani cha Noor, anasema kuwa wazo la kuanzisha shule hiyo lilitokana na jitihada za kupona kutokana na athari za vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, kupitia ujenzi upya wa kisaikolojia na kielimu wa utu wa Mpalestina.
Al-Shakra anaeleza kuwa shule hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuwasaidia watoto, wanawake na wazee kushinda athari za kisaikolojia na kijamii za vita kupitia Qur'ani Tukufu na programu za kielimu, juu ya maghofu na uharibifu uliosababishwa na wavamizi.
Anaonyesha kuwa kituo hicho kwa sasa kina takriban wanafunzi wapatao 800 wa kike na wa kiume wa makundi tofauti ya umri, kuanzia watoto wadogo hadi wazee, baadhi yao wakiwa na zaidi ya miaka sitini, na wanashiriki katika programu maalumu zilizobuniwa kwa mujibu wa mahitaji ya kila kundi.
Kwa mujibu wa al-Shakra, shule hiyo haikomei katika kuhifadhi Qur'ani pekee, bali pia inajumuisha programu za msaada wa kisaikolojia na utoaji wa fursa ya kutoa hisia (emotional evacuation), ambazo zinatekelezwa chini ya usimamizi wa washauri na wanasaikolojia, na zinalenga kupunguza madhara ambayo watoto wamekumbana nayo wakati wa vita.
Anaongeza kuwa programu za shule hiyo zinategemea hadithi za Qur'ani, sira za Masahaba na wahusika wa kihistoria, zikiwa na lengo la kukuza thamani za kimaadili na ustahimilivu miongoni mwa wanafunzi na kumrejesha “mpiganaji wa Mpalestina aliyechoshwa na vita” ili abaki na msimamo na subira.
/3497593