IQNA

Wairani waadhimisha mwaka wa 37 tokea alipoaga dunia Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu Imam Khomeini

17:48 - June 04, 2026
Habari ID: 3482321
IQNA-Wananchi wa Iran wa matabaka mbalimbali wameshiriki katika marasimu mbalimbali ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka wa 37 tangu kufariki dunia Imam Ruhullah Musavi Khomeini (M.A) Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wakazi wa mji wa Tehran, leo walikusanyika katika Haram ya Hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu) kusini mwa Tehran ili kumuenzi na kusisitiza utiifu wao kwa misingi na malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Marasimu ya kumbukumbu ya kifo cha Imam Ruhullah Khomeini yalianza alfajiri kwa wakati wa Tehran ambapo viongozi wa dini walimuombea dua na kumuenzi Mwasisi huyo wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Muda mfupi baadaye, Mohammad Javad Haj Ali Akbari, Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa ya Tehran, alisoma ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei.

Shughuli ya maombolezo ya mwaka huu, ambayo yamefanyika chini ya kauli mbiu ya "Kufungamana na Maimamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Utii kwa Kiongozi," kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma yamehudhuriwa na maelfu ya wananchi pamoja na viongozi na wageni wa ndani na kutoka nje ya nchi.

Imam Ruhullah Khomeini alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 86 mwishoni mwa Juni 3, mwaka 1989. Imam ambaye anatajwa kuwa mmoja wa watu mashuhuri katika historia ya kisasa aliongoza maandamano ya wananchi dhidi ya utawala wa zamani wa Pahlavi wa Iran, ambao ulikuwa muitifaki mkuu wa Marekani.

Aliishi uhamishoni kwa miaka mingi huko Iraq, Uturuki na Ufaransa, ambako aliongoza harakati za mapambano za wananchi kuanzia mashinani na kupelekea kuung'oa madarakani utawala wa kifalme nchini Iran.

3497714

captcha