iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri amewaenzi na kuwatunuku zawadi wanafunzi walioshika nafasi za juu katika mashindano ya hivi karibu ya Qiraa ya Qur'ani Tukufu na Ibtihal.
Habari ID: 3474540    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/11

TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri Sheikh Ahmed el Tayyib, amekosoa jitihada za utumizi wa istilahi ya 'Dini ya Kiibrahimu' kwa lengo la kuziunganisha dini za Kiislamu, Kikristo na Kiyahudi.
Habari ID: 3474533    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/09

TEHRAN (IQNA)- Sheikh Mahmoud Shaltut wa Misri alikuwa miongoni mwa wanazuoni walioanzisha harakati ya kukurubisha madhehebu za Kiislamu na alitoa fatwa ya kihistoria kuhusu Ushia.
Habari ID: 3474491    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/30

TEHRAN (IQNA)- Hujuma dhidi ya msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wakati wa Sala ya Ijumaa huko Kandahar, Afghanistan imelaaniwa vikali na Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar na Mufti wa Misri.
Habari ID: 3474430    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/16

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar Misri na Mufti Mkuu nchini humo wametoa taarifa na kulaani vikali hujuma ya kigaidi ya Ijumaa dhidi ya Msikiti wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia ambapo watu takribani 100 wameuawa.
Habari ID: 3474399    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/09

TEHRAN (IQNA)- Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri anatazamiwza kuitembelea Iraq mwezi ujao.
Habari ID: 3474311    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/18

TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Nchi za Kiislamu (ISBO) na Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar wametangaza azma ya kuandaa kikao cha Idhaa za Qur’ani za nchi za Kiislamu mwezi Februari mwaka 2022.
Habari ID: 3474294    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/14

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema, uhusiano na ushirikiano imara baina ya Chuo cha Kidini cha Qum na cha Al Azhar cha Misri unaweza kuwa na matokeo chanya na yenye faida kwa Waislamu duniani katika kupambana na ukufurishaji na misimamo ya kufurutu mpaka.
Habari ID: 3474107    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/17

TEHRAN (IQNA)- Chuo Kikuu cha Al Azhar kimewatunuku Qur'ani Tukufu wageni katika Maonyesho ya 52 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Cairo, Misri.
Habari ID: 3474072    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/05

TEHRAN (IQNA)- Sheikh Mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri ametuma ujumbe kwa lugha 15 akitaka dunia iwaunge mkono Wapalestina wanaokandamizwa na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473916    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/16

TEHRAN (IQNA)- Sheikh mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri ametoa taarifa na kulaani ‘ugaidi wa Kizayuni’ baada ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel kuwahujumu Wapalestina katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds.
Habari ID: 3473892    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/09

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu ya Al Azhar kwa mara nyingine imesisitiza kuhusu Fatwa yake ya awali kuwa kudungwa chanjo ya COVID-19 au corona hakubatilishi Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473791    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/07

TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar kimetangaza kuwa kudungwa chanjo ya Corona au COVID-19 haitabatilisha Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473713    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/07

TEHRAN (IQNA) – Uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wa kuchunguza jinai za Israel dhidi ya Wapalestina umeungwa mkono na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri.
Habari ID: 3473631    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/08

TEHRAN (IQNA) – Sheikh Ahmed el-Tayeb, mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha al Azhar ametoa wtio wa kusambazwa chanjo ya corona au COVID-19 kwa usawa.
Habari ID: 3473367    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/17

TEHRAN (IQNA) – Imamu Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri amewakosoa vikali wale ambao wanajaribu kuufungamanisha Uislamu na ugaidi.
Habari ID: 3473277    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/20

Sheikh Mkuu wa Al Azhar
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Mkuu wa Al Qur’ani amelaani vikali vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu na kutaja vitendo hivyo vilivyo dhidi ya dini kuwa ni jinai ya kigaidi.
Habari ID: 3473143    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/06

TEHRAN (IQNA) – Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri kimeanzisha kampeni maalumu ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).
Habari ID: 3473126    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/01

TEHRAN (IQNA) – Imamu Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri Sheikh Ahmed EL-Tayeb amekutana kwa njia ya intaneti na Askofu Mkuu wa Canterbury wa Kanisa la Anglikana Justin Welby ambapo wamejadili njia za kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo mbili na kustawisha mazungumzo baina yao.
Habari ID: 3472944    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/09

TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Kimataifa cha Fatwa katika Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri kimetoa taarifa kuhusu uvumizi unaoenezwa kuwa umewadia mwisho wa dunia au qiyamah.
Habari ID: 3472921    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/02