Sayyid Hassan Nasrullah
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, amesema kuwa, harakati hiyo imejiandaa kikamilifu kukabiliana kwa aina yoyote na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kwamba haiwezekani utawala huo uue watu kisha uishi salama.
Habari ID: 2790516 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/31
Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kamanda wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni yataendelea hadi Quds Tukufu ikombolewe.
Habari ID: 2743221 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/22
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, kumeundwa kamati ya uchunguzi kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ukanda wa Gaza.
Habari ID: 1472788 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/13
Kufuatia kuongezeka na kuenea malalamiko ya Wapalestina katika mji wa Quds (Baitul Maqdis) unaokaliwa kwa mabavu, Ghaza na Ukingo wa Magharibi hivi sasa Wapalestina wanaoishi katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu, yaani Israel, nao pia wameandamana.
Habari ID: 1471813 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/10
Ghasia na machafuko mapya yamezuka kati ya askari wa utawala wa kizayuni wa Israel na waandamanaji wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel baada ya utawala huo kufunga Msikiti mtukufu wa al Aqsa.
Habari ID: 1470536 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/06
Sheikh Bilal Shaaban Katibu Mkuu wa chama cha Hizb Tauhid Islami nchini Lebanon amejiunga na wapenda uhuru na haki duniani katika kulaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel kufunga milango ya Msikiti wa Al Aqsa na kuwazuia Waislamu kuswali ndani ya msikiti huo.
Habari ID: 1466340 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/01
Mahmoud Abbas Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameahidi kuchukua hatua za kisheria kuzuia walowezi wa Kizayuni kuuvuamia Msikiti wa Al Aqsa katika Baitul Muqaddas.
Habari ID: 1461999 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/10/20
Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa ushindi wa Ghaza wa mapambano katika vita vya siku 50 na matamshi ya kushindwa utawala wa Kizayuni mbele ya raia waliozingirwa ni ushindi mkubwa na dhihirisho la ahadi na msaada wa Mwenyezi Mungu na ni bishara ya kufikia ushindi mkubwa zaidi.
Habari ID: 1460936 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/10/17
Khalid Mashal Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina Hamas amesema kuwa, usitishaji wowote wa vita unapaswa kufungamana na uondoshwaji mzingiro wa kidhuluma uliowekwa dhidi ya wananchi wa Ghaza.
Habari ID: 1438342 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/11
Leo inasadifiana na Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Hii ni siku ya kupata nguvu upya taifa madhulumu la Palestina na ni siku ambayo inaunganisha nguvu za umma mzima wa Waislamu na kila mpenda haki duniani katika kupambana na utawala wa kibaguzi wa Kizayuni.
Habari ID: 1433171 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/25
Kiongozi Muadhamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba, njia pekee ya kukabiliana na utawala wa kinyama wa Israel, ni kuwepo muqawama wa kutumia silaha wa Wapalestina na kupanuka wigo huo wa mapambano hadi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 1433169 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/25
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa wito kwa taifa la Palestina kuuhami na kuulinda Msikiti wa Al Aqsa.
Habari ID: 1395102 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/04/14
Sambamba na majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuendeleza migogoro katika ardhi za Palestina kwa kuushambulia Msikiti wa kihistoria wa al Aqsa, Uri Ariel Waziri wa Makazi wa utawala huo ghasibu ameukoleza zaidi mgogoro huo kwa kuingia ndani ya msikiti mtakatifu wa al Aqswa.
Habari ID: 1388191 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/03/17